LIVE STREAM ADS

Header Ads

IDADI YA MAUZO SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM YASHUKA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for SOKO LA HISA DAR IMAGENa James Salvatory - BMG Dar
Idadi ya mauzo katika soko la hisa Jijini Dar es salaam (DSE) imeshuka kwa asilimia 34% na kufikia TZS 2.2 Bilioni kutoka TZS 3.3 Bilioni wiki iliyopita.

Akizungumza mwishoni mwa wiki na wandishi wa habari jijini Dar es salaam, meneja mwandamizi wa soko hilo,Mery Kinabo, alisema idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zimeshuka kwa asilimia 42 hadi Milioni 1.3 kutoka Milioni 2.2  na Kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni CRDB kwa asilimia 41% DSE kwa asilimia 36% NMB kwa asilimia 9%.

Aidha Kinabo alisema ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa 0.03% na kufika Trilioni 22.7 kutoka Trillioni 23.4. huku Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umeshuka kwa 0.01% na kufika Trilioni 8.3 kutoka Trillioni 8.4.

Aliongeza kuwa Viashiria (Indexes) Sekta ya viwanda (IA) wiki hii imeshuka kwa pointi 66.10 baada ya bei za hisa za TBL kushuka kwa 2.13% huku Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imeshuka kwa pointi 7.83 baada ya bei kushuka kwenye kaunta za DSE kwa 33.73% na DCB 14% na Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii iko vilevile baada ya bei za hisa za Swissport kubaki TZS 3,543.02.

Kwa upande wa Shindano la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (DSE Scholar Investment Challenge 2016) mshindi wa kwanza Godfrey Pantaleo Makweka  kutoka Institute of Accountancy Arusha, Wa pili ni Benson Humphrey kutoka  Sokoine University of Agriculture Na wa tatu Frank Kigodi kutoka  University of   Dodoma.

No comments:

Powered by Blogger.