SERIKALI YAKANUSHA VIKALI KUWA MMOJA WA WALIOFUKIWA NA KIFUSI MKOANI SHINYANGA ALILIWA.
Na:Shaban Njia,Kahama
SERIKALI imekanusha vikali tetesi zilizozagaa katika mji wa Kahama Mkoani Shinyanga kuwa mmoja wa Wahanga waliofukiwa katika Mgodi wa Machimbo madogo ya Nyangarata Mkoani humo aliliwa na wenzake baada ya njaa kuwazidi.
Akizungumza muda mfupi baada ya Mwili wa Marehemu Musa Supana ambae alifariki katika machimbo hayo na mwili wake kupatikana usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba na nusu usiku, Kaimu Kamishna wa Madini Nchini Ally Samaje alisema kuwa uvumi huo si wa kweli na kuongeza kuwa mwili huo umetolewa ukiwa hauna majeraha yeyote.
Alisema kuwa zoezi la kuutoa Mwili huo lilifanywa na Wachimbaji wadogowadogo wa Mgodi huo huku Wizara ya Nishati na Madini ikiwa kama msimamizi wa zoezi hilo kwa muda wote tangu zoezi la uokoaji lilipoanza.
Aidha Naibu huyo alisema kuwa jumla ya Vijana waliofanikisha kuutoa Mwili wa Marehemu huyo walikuwa 25 huku wakikadiriwa kutumia zaidi ya shilingi millioni 13 ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo la uokoaji linafanikiwa na kuongeza kuwa mwili huo ulikuwa zaidi ya mita 120 kwenda chini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mgodi mdogo wa Shigitwa (SHIGOMIKO) Hamza Tandiko alisema kuwa wanashukuru mungu kwa mwili wa Marehemu Supana kupatikana na kuongeza kuwa sasa wanasubiri daktari kwa ajili ya kuupima kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwao Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.
“Mpaka kufikia jana sisi kama Wachimbaji wadogowadogo wa Nyangalata tumetumia zaidi ya shilingi milioni 13 kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uokaji hali ambayo kwa sasa kila mmoja hana fedha kwani tulikuwa tukijichangisha wenyewe”. Alisema Tandiko.
Aidha Tandiko alisema kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika Viongozi wa Chama cha Wachimbaji wadogowadogo Mkoa Wa Shinyanga (SHIREMA)watakaa kwa pamoja ili kuona jinsi ya kuwasadia Wahanga waliopo Hospitali ya Wilaya ya Kahama ikiwa ni pamoja na kutoa mawasiliano yao ili wasamaria watakagushwa kuwachangia waweze kufanyo hivyo.
Siku tano baada ya Wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Nyangalata kuwaoko wenzao watano kati ya sita waliofukiwa na kifusi na kukaa chini kwa muda wa siku 41 na mmoja kufariki dunia kutokana na njaa, kulizuka uvumi kuwa wahanga walifanikiwa kuwa hai kwa siku zote hizo baada ya kumla mwenzao.
No comments: