LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHADEMA WATAKA HUDUMA ZA AFYA KUBORESHWA KATIKA VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI MKOANI MWANZA ILI KUPUNGUZA ONGEZEKO LA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA SEKOUR TOURE.

Grace Tendega ambae ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa (Kushoto) akizungumza baada ya kutembelea Wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Tour hii leo February 20,2016. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Chadema Mkoani Mwanza Susan Masele.

Katika ziara hiyo, Tendega ameishauri Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za afya katika Vituo vya afya pamoja na Zahanati ili kupungumza wingi wa wagonjwa katika Hospitali hiyo ya Sekou Toure.

Amebaini changamoto ya ukosefu wa vitanda katika wodi za akina mama katika hospitali hiyo pamoja na upungufu wa dawa huku pia suala la upatikanaji wa damu likiwa ni changamoto nyingine ambapo ameshauri wananchi kuwa na desturi ya kujitolea uchangiaji wa damu ili kuokoa maisha ya wahitaji.

Nae Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) Susan Masele, amesema ataishinikiza Serikali ili kuhakikisha inaongeza bajeti yake katika Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ili kukabiliana na changamoto za kiafya nchini ikiwemo kupambana na mapungufu yaliyopo katika Hospitali ya Sekour Toure Mkoani Mwanza.

"Tunashukuru mbunge wa Viti Maalumu kututembelea hospitalini hapa na kutuletea mahitaji mbalimbali ambayo yatatusaidia katika kipindi hiki". Ameeleza mmoja wa wagonjwa katika wodi ya akina mama baada ya kupokea baadhi ya mahitaji ikiwemo juice kutoka kwa mbunge Masele.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Onesmo Rwakyendela amekiri baadhi ya mapungufu katika hospitali hiyo ambapo amesema kuwa juhudi zinazidi kufanyika ili kupambana na changamoto hizo ambazo ni pamoja na uchache wa vitanda katika wodi ya akina mama kujifungulia, ambapo changamoto hiyo inatokana na wingi wa akina mama wanaofika hospitalini hapo kwa ajili ya ya kupata huduma.

Ziara hiyo imejiri kabla ya Uzinduzi wa Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoani Mwanza Susan Masele, iliyopo katika Mtaa wa Ghana, Kata ya Nyamanoro Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) Susan Masele
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Onesmo Rwakyendela
Grace Tendega ambae ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa akimjulia hali mmoja wa wagonjwa.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) Susan Masele akimjulia hali mmoja wa wagonjwa.
Ziara ya Viongozi wa Chadema kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure.
Ziara ya Viongozi wa Chadema kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Onesmo Rwakyendela baada ya kupokea ugeni kutoka Chadema.
Picha Za Uzinduzi wa Ofisi BONYEZA HAPA.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.

No comments:

Powered by Blogger.