LIVE STREAM ADS

Header Ads

HABARI PICHA, RAIS MAGUFULI ALIVYOTIKISA JIJI LA MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Jana Rais John Pombe Magufuli (kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi Jijini Mwanza. 
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela.
Pia Rais Magufuli ameweka Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa daraja la Watembea kwa Miguu la Furahisha Jijini Mwanza.

Pamoja na shughuli hizo, pia Rais Magufuli amehuhutubia umati mkubwa wa wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Rais Magufuli ameendelea kusisitiza kwamba, ataendelea kutumbua mafisadi pamoja na watumishi hewa ambayo walikuwa wakiligharimu taifa fedha nyingi ambapo zaidi ya shilingi bilioni 18 zilikuwa zikitumika kuwalipa zaidi ya watumishi hewa elfu kumi na mbili, ambapo fedha hizo sasa zinasaidia utekelezaji wa mpango wa Elimu bure nchini.

Amesema baadhi ya viongozi walikuwa wakitumia sherehe mbalimbali ambazo amezifuta ikiwemo sherehe za uhuru kama njia ya kula fedha na ndiyo maana aliamua kufuta sherehe hizo na fedha zake kujenga upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi Jijini Mwanza.

Aidha Rais Magufuli ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa nchini Takukuru kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na viongozi wa serikali mkoani Mwanza, kuhakikisha mali zote za Chama cha Ushirika Nyanza zilizouzwa ikiwemo majengo, zinarejeshwa kwa wananchama na wahusika wanachukuliwa hatua za kisheria.
Ufunguzi wa upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi Jijini Mwanza.
Rais Magufuli akipokea taarifa ya ujenzi wa daraja la Watembea kwa Miguu la Furahisha Jijini Mwanza
Rais Magufuli akihutubia uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akisalimia wananchi katika mkutano huo
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, akisalimia wananchi
Mbunge wa Jimbo la Buchosa na Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Charles Tizeba, akisalimia katika mkutano wa Rais Magufuli Jijini Mwanza
Msanii Christian Bella akitumbuiza kwenye mkutano huo, Pia Juma Nature na wasanii wengine walitumbuiza
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini Tanroad, Mhandisi Patrick Mfugale, akitoa taarifa kwenye mkutano huo
John Shibuda, akisalimia wananchi katika mkutano wa Kiserikali, wa Rais Magufuli kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, jana
Viongozi mbalimbali
Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kiserikari wa Rais Magufuli, kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza
Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa Rais Magufuli Jijini Mwanza
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi

No comments:

Powered by Blogger.