LIVE STREAM ADS

Header Ads

MUUNGANO WA MACHINGA MKOANI MWANZA WATOA YA MOYONI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga mkoani Mwanza, Said Tembo (kulia) akizungumza na Mhariri wa Lake Fm Mwanza, Amos Gomba (kushoto) kuhusiana na kikao cha kamati ya uongozi wa umoja huo kinachofanyika hii leo. Katikati ni Tano James, Mjumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama, Muungano wa Machinga Mwanza.
#LakeFmHabari
Muungano wa wafanyabiashara ndogondogo Machinga mkoani Mwanza, umetaka iwepo mipango madhubuti ya kuwapanga wafanyabiashara hao katikati ya Jiji la Mwanza badala ya kuwatimua.

Mwenyekiti wa Muungano huo, Said Tembo, ameyasema hayo wakati akizungumza na Lake Fm juu ya mikakati iliyopo kuelekea mwaka 2017 ili kuhakikisha machinga wanafanya biashara zao bila kuvunja taratibu zilizowekwa.

Tembo amesema hivi karibuni haikuwa sahihi viongozi mkoani Mwanza, kuwaondoa machinga katikati ya Mji huku bado kukiwa hakuna maeneo ya kutosha na yenye miundombinu bora kwa wao kufanyia biashara.

Disemba tatu mwaka huu, machinga wote waliondolewa katikati ya Jiji la Mwanza ambapo zoezi hilo liliratibiwa na halmashauri ya Jiji la Mwanza, Manispaa ya Ilemela, ofisi za wakuu wa wilaya za Nyamagana na Ilemela kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kabla ya zoezi hilo kuzuiliwa na Rais John Magufuli na hivi sasa machinga wanaendelea na biashara zao kama kawaida katikati ya mji.
Mhariri wa Lake Fm Mwanza, Amos Gomba (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga mkoani Mwanza, Said Tembo (kulia) kuhusiana na kikao cha kamati ya uongozi wa umoja huo kinachofanyika hii leo. Katikati ni Tano James, Mjumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama, Muungano wa Machinga Mwanza.
Picha na BMG

No comments:

Powered by Blogger.