LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Kwamba tarehe 10.01.2016 majira ya saa 17:00hrs katika kijiji cha Igombe kata ya Bugogwa wilaya ya Ilemela jiji na mkoa wa Mwanza, mtu mmoja mwanamume aliyejulikana kwa jina la Edson Paul miaka 24, msukuma na mkazi wa Buswelu, aliuawa na kundi la watu waliojichukulia sheria mkononi baada ya kutenda wizi kwenye duka la  mihamala ya fedha ya njia ya mtandao.

Inadaiwa kuwa marehemu alifika kwenye duka la mihamala ya fedha (P-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money) na kumwomba mhudumu wa duka hilo aitwaye Bahati Nyagawa miaka 18, amtumie fedha kwa njia ya M-pesa kiasi cha tsh 295,000/=, kwenye namba yake ya simu, inasemekana kuwa baada ya kutumiwa fedha hizo kwenye namba yake ya simu mhudumu wa duka hilo bBahati Nyagawa aliomba kupatiwa fedha hizo (cash) ambazo alimhudumia, marehemu alionekana hakuwa na fedha na alitaka kutoroka eneo la tukio

Inasemekana kuwa wakati anataka kutoroka eneo la tukio, wananchi waliokuwa maeneo ya karubu walijitokeza na kumkamta  na kuanza kumshambulia kwa mawe na marungu sehemu mbalimbali za mwili wake hadi umauti ukamkuta papo hapo.

Jeshi la polisi linamshikilia mhudumu wa duka hilo Bahati Nyagawa kwa mahojiano zaidi, aidha hakuna mtu mwingine yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa mazishi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa rai kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza akiwataka kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni ukiukwaji wa haki za binadamu, bali wafuate utaratibu pindi wanapomkamata mhalifu ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake. aidha anawataka vijana kufanya kazi za halali na kuacha tabia za uhalifu kitendo ambacho ni kosa la jinai. endapo marehemu asingefanya tukio hilo haya yaliyomkuta yasingempata.

Pia mnamo tarehe 11.01.2017 majira ya saa 01:30hrs, usiku katika maeneo ya Kiss Pub kata ya Kirumba wilaya ya Ilemela jiji na mkoa wa Mwanza, askari wakiwa doria na misako walimkamata mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la James Peter miaka 22, mkazi wa misungwi akiwa na noti bandia nne za shilingi elfu kumi ya Tanzania zenye thamani ya jumla ya tsh, 40,000/=, zenye namba 1. BX 98546121, 2. BX 9851404, 3. BX 9851407 na 4. BX 320598, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Awali askari walipokea taarifa kutoka kwa raia wema juu ya uwepo wa kijana mwenye fedha bandia mahali hapo, askari walikwenda haraka hadi eneo la tukio na kufanya upelelezi kuhusiana na taarifa hizo na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa tajwa hapo juu. tuhumiwa yupo katika mahojiana na jeshi la polisi, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi wa jiji na mkoa wa mwanza akiwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwakamata wahalifu katika mkoa wetu wa mwanza, lakini pia anawataka wananchi kubadilika na kufanya kazi zilizo halali.

metolewa na,
DCP: Ahmed Msangi 
Kamanda wa polisi (M) Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.