LIVE STREAM ADS

Header Ads

JAJI WARIOBA AVUNJA UKIMYA KUHUSIANA NA VITA YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory
Serikali imetakiwa kuwekeza zaidi katika kutoa elimu kuanzia ngazi ya  familia hadi kitaifa ili kukabiliana na janga la dawa za kulevya.

Akizungumza jana katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Jaji Mstaafu Joseph  Warioba, alisema vita ya dawa za kulevya ni shirikishi katika jamii nchini.

Jaji Warioba alisema serikali inapaswa kuelimisha jamii juu ya madhara dawa za kulevya iwemo ulimaji wa bangi ambapo katika eneo la vijijini zao hilo limekuwa la kawaida kulimwa na wananchi kutokana na kutojua madhara yake.
Jaji Warioba alisema ni lazima jamii ipewe elimu na njia mbadala ya kuishi pasipo kutumia dawa za kulevya sambamba na juhudi za kuzuia dawa hizo zisiweze kupenya mipakani na kuingizwa nchini.

"Katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, ni vyema wanasiasa wakaachana na itikadi zao na badala yake wakaweka nguvu pamoja katika kukabiliana na janga hilo". Alisisitiza Warioba.

No comments:

Powered by Blogger.