LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAADHIMISHO YA WIKI YA KINYWA NA MENO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,  Albert Msovela, akizungumza na madaktari wa Kinywa na Meno kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam (pichani hawapo) wakati walipofika Ofisini kwake na kujitambulisha katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya Wiki ya Kinywa na Meno ambapo kilele ni machi 20, Dodoma na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana.

"Napenda kutoa shukrani za kipekee na kwaniaba ya Mkoa wangu  kwa jinsi mnavyo jitowa katika kuwahudumia ndugu zetu, watoto wetu na mgeweza kwenda sehemu nyingine lakini kwa mfululizo wa miaka  mitatu mnakuja kututembelea na kutowa huduma, misaada na elimu ya jinsi ya kutunza afya ya kinywa na meno na sasa kunamabadiliko makubwa tofauti na mara ya kwanza mlipofika na baada ya hapo wengi walijitokeka katika kusaidia watoto hao". Alisema.
Madaktari wa Kinywa na Meno wakikaribishwa na watoto wa Shule ya Msingi Buhangija Mkoani Shinyanga kwa wimbo
Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salamu, Conrad Mselle akitowa Elimu ya upigaji mswaki wa Kinywa na Meno leo mbele ya wanafunzi wa shule hiyo katika kuelekea kilele cha Maadhimisho yatakayofanyika machi 20, mwaka huu Dodoma, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana  
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dr. Lorna Carneiro akizungumza na wanafunzi hao
Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya akifungua  wiki ya kinywa na Meno leo katika Shule ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jumuishi ya Kata ya Buhangija Mkoani Shinyanga
Maktari Bingwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Habiba Madjapa (kulia) na Dr Arnold Mtenga (katikati) wakijadiliana na Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno, Tanzania Dr. Lorna Carneiro (kushoto)
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,  Albert Msovela (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na madaktari hao

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,  Albert Msovela (kulia ) akikabidhiwa flana na  Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dr. Lorna Carneiro mara walipofika na msafara wake kwa lengo la kujitambulisha
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno, Tanzania Dr Lorna Carneiro (kushoto) akizngumza jambo wakati walipofika yeye na msafara wake kumsalimia Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,  Albert Msovela (kulia) katikati ni Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,  Albert Msovela (katikati aliyevaa koti) akizungumza na madaktari hao (kulia).
Na Khamis Mussa

No comments:

Powered by Blogger.