LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KUHUSU TETEMEKO LA ARDHI JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

#LakeFmHabari
Wakazi wa jiji la mwanza na maeneo jirani wameingiwa na hofu baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi majira ya saa saba adhuhuri hii leo.

Baadhi ya waliokumbwa na hofu kubwa ni wale waliokuwa katikati ya mji hususani maofisini kwenye majengo marefu ikiwemo mtaa wa liberty ambao walianza kukimbia ovyo wakitoka nje.

Hata hivyo tetemeko hilo halikusababisha madhara yoyote jijini mwanza ambapo wananchi wameomba mamlaka husika kutoa tahadhari za matukio ya aina hiyo ili kuchukua tahadhari mapema.

Kwa mujibu wa wakala wa jiolojia nchini, asilimia kubwa ya watu wanaotaharuki na kukimbia ovyo wakati wa tukio la tetemeko la ardhi, ndio huumia ama kupata madhara makubwa hivyo wananchi wanashauriwa kuwa watulivu katika kipindi hicho na kutafuta pahala salama pa kujihifadhi.
Usikose kusikiliza #LakeFmHabari hii leo saa 11:00 jioni.

No comments:

Powered by Blogger.