LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mradi wa kujengea uwezo wataalam na wakulima wapata wafanikio makubwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Marco Ndonde akifungua mkutano wa majadiliano ya wadau kuhusu mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha umwagiliaji uliyofanyika jijini Dodoma.
Ukombeso Emmanuel ambaye ni Afisa Kilimo kutoka Manyara akiongea na waandishi wa habari (hawapo katika pichani) kuhusu faida iliyopatikana kutokana na mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha umwagiliaji.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya majadiliano ya kubadilishana mawazo kuhusu mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za Kilimo cha Umwagiliaji iliyofanyika jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Imeelezwa kuwa, mradi wa kujengea uwezo kwa wakulima na wataalamu katika Kilimo cha Umwagiliaji nchini umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia matumizi ya muongozo yakinifu wa umwagiliaji na Mafunzo ya uendeshaji na matunzo ya skimu za umwagiliaji katika maeneo ya mfano yaliyo chaguliwa na mradi huo.

Hayo yalielezwa Januari 28, 2020 Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Marco Ndonde alipokuwa akifungua warsha ya wadau na wataalam wa kilimo yenye lengo la kubadilishana mbinu zitakazotumiwa kufanya mafanikio ya mradi kuwa endelevu ili kuwezesha ukuzaji wa sekta ya umwagiliaji kote nchini.

Ndonde alisema kuwa, mradi huo umekuwa wa mafanikio kwa kiasi kikubwa kutokana na wadau wa kilimo hicho kutumia mwongozo wa umwagiliaji kwa umakini katika kutekeleza shughuli zote za kilimo cha Umwagiliaji.

Afisa Kilimo kutoka Ofisi za Kilimo cha Umwagiliaji Manyara, Lukombeso Emmanuel, alisema Serikali amefanya uwekezaji mkubwa katika eneo la umwagiliaji kupitia mradi huo jambo ambalo limewawezesha wakulima wenyewe kuweza kupata uelewa hususan katika eneo la matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji jambo ambalo awali muamko ulikuwa mdogo.

"Kwa upande wetu sisi kama wataalam katika ngazi zote tumejengewa uwezo juu ya uibuaji, , utekekelezaji, uendeshaji na mafunzo pamoja na ufuatiliaji na tathmin kwa kufuata mwongozoyakinifu wa Umwagiliaji na namna ya kuwawezesha wakulima kufanya shughuli zao kufuata Mwongozo huo" alisisitiza Lukumbeso.

Pamoja na mafanikio hayo mradi umekuwa na changamoto mbalimbali kwa wakulima kama vile uelewa mdogo kuhusu Sheria, kanuni na Miongozo ya Kilimo cha Umwagiliaji jambo ambalo linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu kupitia kuitambulisha rasmi Sheria ya Umwagiliaji kwa wadau mbalimbali na kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Awamu hiyo ya pili ya mradi wa kujengea uwezo wakulima katika Kilimo cha Umwagiliaji unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

No comments:

Powered by Blogger.