LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mashirika yanayotetea wafanyakazi wa majumbani yatakiwa kutoa elimu ya uwajibikaji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Muungano wa Mashirika yanayojihusisha na Watoto na Wafanyakazi wa Nyumbani (TCDWC) umeombwa kuhakikisha mashirika yanayotoa huduma kwa Watoto wanaofanyakazi za nyumbani mbali yalikutoa elimu juu ya haki zao lakini pia iwakumbushe wajibu wao katika kutimiza majukumu yao.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa majadiliano katika warsha ya siku moja ya kupiga vita ukatili wa majumbani iliyoandaliwa na shirika la TCDWC kwa kushirikiana na taasisi ya OJADACT kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Mwanza,
Akichangia mjadala huo mwandishi wa habari Tonny Alphonce aliutaka Muungano wa mashirika yanayojihusisha na watoto na wafanyakazi wa nyumbani kuongea na mashirika wenza kuangalia namna ya kuwapatia elimu juu ya utendaji wa kazi wa wafanyakazi wa nyumbani na kuacha kujikita zaidi katika kuwafundisha juu ya haki zao ambao wengi wao hupigania haki zao na kusahau wajibu wao.

“Wafanyakazi wa majumbani ni kweli wananyimwa baadhi ya haki zao za msingi na sababu kubwa ni kwamba wengi wao hawana elimu kwa maana hiyo utendaji wao wa kazi pia sio mzuri unakuta mwajiri kila siku lazima atoe darasa kwa dada wa kazi hii sio sawa kama tunataka nao waangaliwe kama wafanyakazi wengine basi mashirika yanatakiwa kuwajengea uwezo pia wa kiutendaji ili kupunguza mgongano ulipo.”alisema Tonny.

Naye mwandishi wa habari Clara Matimo amesema wazazi wa wasichana wanaofanyakazi za nyumbani nao wanashiriki katika kuwafanyia ukatili mtoto kwa sababu wengi wao humtaka mwajiri kuhakikisha anatuma mshahara wa binti wa kazi kwao kila mwezi na kumwacha binti bila pesa yoyote.

Amesema kutokana na kitendo hicho cha mtoto kufanyakazi bila kulipwa hupelekea kurubuniwa kimapenzi kiurahisi kutoka kwa watu wanaomzunguka na kujikuta anapata ujauzito au magonjwa ya zinaa na mwisho huachichwa kazi pale inabobainika kajiingiza katika mahusiano.
Akijibu baadhi ya hoja za washiriki, Glory Ndaki Mwanasheria na mdau wa kutetea haki za Watoto majumbani amesema licha ya mapungufu waliyonayo wafanyakazi wa majumbani lakini waajiri wengi wanakiuka sheria za kazi na sheria za mtoto katika kuwapangia majukumu wafanyakazi wa ndani.

Glory amesema kuna mikataba mingi ya kimataifa ambayo Tanzania iliridhia pamoja na sheria mbalimbali zinazomlinda mtoto lakini zimekuwa zikivunjwa na waajiri ama kwa kujua au kwa kutozijua hivyo aliwataka wanahabari kuhakikisha watoa elimu hiyo.

Akizungumzia vitendo hivyo vya ukatili,Mratibu wa shirika hilo la TCDWC Bw George Leornard amesema bado kuna vitendo vingi vya ukatili vinaendelea kufanyika katika jamii hivyo ni wajibu wa wana Habari kufichua na kuielimisha jamii juu ya vitendo hivyo.

”Mnaweza kuona namna tatizo lilivyokubwa,kwa mwezi mmoja wa Agosti mwaka huu tumepokea kesi 30 ambazo zinahusiana na vitendo vya ukatili kwa wafanyakazi wa nyumbani na taarifa hizi ni kutoka hapa Mwanza na matukio haya yamefanyika wilaya za Nyamagana,Ilemela na Magu”.Alisema Leornard

Amesema katika kesi nyingi ambazo wamezipokea malalamiko mengi ni upande wa mshahara kutokulipwa kwa wakati au kunyimwa kabisa pamoja na kufanyishwa kazi ngumu pamoja na manyanyaso ya kingono na kimwili.

Leonard amewata waandishi wa habari kutumia mafunzo hayo vyema na kwenda kuisaidia jamii wakiwemo wazazi wanaotoa Watoto wao kwenda kufanyakazi mjini wafahamu vitu vya msingi ambavyo mwajiri anatakiwa kufanya kabla ya kumchukua mtoto ukiwemo mkataba wa kazi na kuyafahamu amazingira ambayo mtoto anaenda kufanyakazi.

Edwin Soko mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari wa kupiga Vita Matumizi ya Dawa Za Kulevya na Uhalifu Tanzania amewataka wanahabari kutumia mafunzo hayo kwa kuleta mabadiliko katika jamii na kuhakikisha vitendo vya ukatili wa wanayakazi wa ndani vinaisha au vinapungua kwa kiwango kikubwa kupitia maandiko mbalimbali.
ILO ilipitisha Mkataba namba 189 mwaka 2011 Mkataba huu unabainisha viwango vya chini vya kimataifa vya ajira vinavyolenga kuleta kazi ya staha kwa wafanyakazi wa majumbani.

Haki za msingi zilizo ainishwa kwenye mkataba namba 189 inasema hairuhusiwi mtoto mwenye umri chini ya miaka 15 kufanya kazi za majumbani. Mtoto mwenye umri unaozidi ule ulioainishwa hapo juu apewe ruhusa ya kumaliza elimu ya msingi na kujiendeleza au kupata mafunzo ya kazi.
Na Tonny Alphonce,Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.