LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mabingwa MWALIMU DOTO CUP 2021 wapatikana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Michuano ya waalimu ya 'Mwalimu Doto Cup 2021' imefikia tamati katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo timu ya soka ya waalimu kutoka Kata ya Namonge imetwaa ubingwa baada kuitandika timu ya waalimu kutoka Kata ya Butinzya kwa goli 3-0 katika uwanja wa Shule ya Sekondari Ushirombo.

Upande wa mpira wa pete, timu ya waalimu kutoka Kata Runzewe Magharibi wameibuka mabingwa baada ya kuwatandika wenzao wa Kata ya Katente kwa magoli 17-14. Michuano hiyo iliasisiwa na mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini.
Timu ya Namonge (jezi nyeusi) ikipepetana na timu ya Butinzya (jezi ya kijani) katika fainali za michuano ya Mwalimu Doto Cup 2021 wilayani Bukombe.
Timu ya Namonge (jezi nyeusi) ikipepetana na timu ya Butinzya (jezi ya kijani) katika fainali za michuano ya Mwalimu Doto Cup 2021 wilayani Bukombe.
Waamuzi katika mchezo wa fainali uliopigwa Oktoba 04, 2021.
Mwasisi wa michuano ya Mwalimu Doto Cup, Doto Biteko (wa pili kushoto) akikagua kikosi cha timu ya Butinzya. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya Bukombe, Said Nkumba.
Mwasisi wa michuano ya Mwalimu Doto Cup, Doto Biteko (wa pili kushoto) akisalimiana na wachezaji.
Mwasisi wa michuano ya Mwalimu Doto Cup, Doto Biteko (kushoto) akisalimiana na wachezaji wa timu ya Namonge. 
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.