LIVE STREAM ADS

Header Ads

Uzuri wa Tanzania (S02-E07) Ulipofikia ujenzi wa Soko Kuu jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mradi mkubwa wa ujenzi wa soko kuu jijini Mwanza unaendelea vyema licha ya muda uliopaswa kukamilika kuisha ambapo mradi huo ulioanza Julai 2019 ulipaswa kukamilika Aprili 2022.

Hata hivyo inaelezwa kuwa mradi umefikia zaidi ya asilimia 50 ya utekelezaji wake na hatua iliyosalia ikiwa mipango yote itakwenda sawa, basi mkandarasi anaweza kukamilisha kazi mwishoni mwa mwaka huu.

Miongoni mwa huduma zitakazopatikana baada ya kukamilika kwa mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 23 ni kujumuisha wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa kukiwa na yumba vya maduka zaidi ya 400, vizimba kwa ajili ya wafanyabiashara wa nafaka, mbogamboga na matunda zaidi ya 500 pamoja na fursa nyingine nyingi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.