LIVE STREAM ADS

Header Ads

TCCL kuboresha zaidi huduma za mawasiliano, mkongo wa taifa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL) imejipanga kupanua na kuboresha zaidi mkongo wa taifa wa mawasiliano ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi mjini na vijijini.

Hayo yamebainishwa na Alhamisi Aprili 04, 2024 jijini Mwanza na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Zuhura Muro wakati wa akizungumza kwenye hafla ya kuwafuturisha waumini wa dini ya kiislamu iliyoandaliwa na shirika hilo.

Muro amesema upanuzi wa mkongo wa taifa wa mawasiliano ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchini huku ukitarajiwa kuleta tija kwa wananchi ikiwemo kuimarisha huduma ya mawasiliano hususani intaneti yenye kasi (fiber).

“Shirika lina jukumu kubwa kuhakikisha mawasiliano yanapatikana nchini hivyo lina wajibu wa kuendelea kupanua na kuboresha miundombinu yake kwani ni shirika linalotegemewa na wananchi pamoja na wadau wengine wa mawasiliano” amesema Muro.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mhandisi Peter Ulanga amesema upanuzi na uboreshaji wa mkongo wa taifa wa mawasiliano utasaidia kuleta chachu kwa wananchi katika Nyanja mbalimbali ikiwemo za kiuchumi, kijamii na kiusalama.

“Tunampongeza Rais Dkt. Samia Samia Suluhu kwa juhudi zake za kuhakikisha shirika linafanya uwekezaji mkubwa ili kuifanya Tanzania ya kidijitali kufikiwa huku pia shirika likiendelea kuimarisha miundombinu hatua itakayosaidia kuleta unafuu wa gharama za mawasiliano kwa wananchi ” amesema Ulanga.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda ametoa rai kwa TTCL kuendelea kuboresha huduma za mawasiliano ili kuwafikia wateja wengi zaidi.

Masala amesema “kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, tunaendelea kulinda miundo mbinu ya mawasiliano inayoboreshwa nchini ikiwemo mkongo wa taifa wa mawasiliano ili kufikia matarajio ya wananchi kupata mawasiliano bora.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Zuhura Muro akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu TTCL, Mhandisi Peter Ulanga akitoa salamu wakati wa hafla hiyo ya Iftar.
Katibu Baraza la Masheikh Mkoa Mwanza, Sheikh Othman Masasi akitoa salamu za shukurani kwa TTCL kwa niaba ya Sheikh wa Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke za shukurani kwa TTCL kwa kuandaa futari hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akitoa salamu kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda.

No comments:

Powered by Blogger.