LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Rais Samia kuboresha Reli ya Kaskazini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda Januari 8, 2025 amekutana na kuzungumza na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa juu ya ombi la kuboresha reli ya Kaskazini (Tanga - Arusha) ili kuboresha huduma za utalii mkoani Arusha.

Makonda amesema kuboreshwa kwa reli hiyo pamoja na kujengwa kwa bandari kavu mkoani Arusha kutaondoa wingi wa malori ya mizigo barabarani pamoja na kusaidia barabara kudumu kwa muda mrefu.

Baada ya mazungumzo hayo, Waziri Mbarawa ameridhia ombi hilo na amesema mkoa huo ni muhimu kwa utalii na uchukuzi ukiwa wa tatu kwa miruko ya ndege nchini ambapo serikali imetenga Bilioni 11 za kufunga taa katika uwanja wa ndege wa Arusha zoezi litakaloanza hivi karibuni.
KAZI INAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.