ALIEKUWA MTANGAZAJI WA RADIO METRO NA KWA SASA RADIO KWIZERA ATOA YAKE YA MOYONI.
![]() |
Dotto Jasson Bahemu alipokuwa Radio Metro. |
Bahemu ambae alimeguka kutoka katika Familia ya Metro FM mwanzoni mwa mwaka jana ameelezea hisia zake wakati akiwa Radio Metro na namna alivyoshirikiana na team ya Metro FM vizuri huku Sifa na Utukufu akizipeleka kwa Alphonce Tonny Kapela aka Dk.Tonny ambae anasema aliweza kumfanya ajifunze vitu vingi ambavyo vimemfikisha hapo alipo hivi sasa.
Hongera sana Bahemu kwa kuelezea hisia zako maana ni wachache wenye moyo kama wako, japo ulipata kigugumizi kuweka bayana ni wapi uliwahi kufanya kazi na Dk.Tonny. Lakini hiyo haina tatizo maana Mtanzania Media imewasaidia Wasomaji kwa hilo. Na hiki ndicho alichokiandika Dotto Jasson Bahemu June 20 Mwaka huu kupitia ukurasa wake wa Facebook kumhusu Alphonce Tonny Kapela aka Dk.Tonny kutoka Radio Metro baada ya kumsikiliza kwa mara nyingine tena...
Huyu Jamaa anaitwa Alphonce Tonny
Kapella, nimewahi kufanya naye kazi sehemu flani, kisha niliondoka
nikahamia kwingine. Pamoja na mm kuondoka KIUKWELI nilijifunza mambo
mengi kutoka kwake ambayo mpaka leo YAMENIJENGA katika maisha binafsi
na kazini pia.
Nilikaa muda mrefu bila kusikiliza kazi zake, lakini
wiki hii nimepata nafasi ya kumfuatilia sana, NIMEGUNDUA haukuwa wakati
muafaka kwangu kuacha kufanya kazi na Tonny, nimegundua bado nilikuwa
nahitaji kujifunza mambo mengi sana kutoka kwa Tonny, Tonny yuko Deep
saana, na ninaamini kuna siku ataenda mbali zaidi ya hapo alipo kwa
sasa, KEEP IT UP BROOO, nafikiri mtakubali nachosema.
No comments: