LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAJINA YA VIGOGO WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUTAJWA HADHARANI.

Mwenyekiti wa OJADACT Edwin Soko.
Chama cha Waandishi wa Habari wanaopinga Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uharifu nchini OJADACT kimeitaka Serikali kuwataja na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya hapa nchini na kusababisha maisha ya Watanzania hususani vijana kuangamia.

Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko ameyasema hayo hii leo Mkoani Mwanza yalipo Makao Makuu ya Chama hicho, wakati akitoa tamkoa la Chama ikiwa ni siku moja kabla ya kuadhimisha maashimisho ya Siku ya Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo yataadhimishwa Kesho Kote Ulimwenguni.

Soko amesema kuwa kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikikaa kimya bila kuwataja mapapa ambao wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya hapa nchini, licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa Majiana ya watu hao yapo na yanafahamika huku wengi wao wakisadikiwa kuwa ni vigogo wa Serikali na pengine ndiyo sababu ya inayofanya Serikali kutoyaweka hadharani majina hao.
Mwenyekiti wa OJADACT Edwin Soko.
Aidha amesema kuwa OJADACT inaendelea na uchunguzi wake juu ya kuhakikisha inawatambua watu (Vigogo) wanaojihusisha na biashara ya uingizaji na usafirisha wa dawa za kulevya hapa nchini na hivyo kuyaweka hadharani majina hayo kama Serikali itashindwa kufanya hivyo hatua ambayo amesema kuwa itasaidia kupambana na vita ya dawa za kulevya ambayo imeshika kasi hapa nchini na kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza kwa uingizaji na usafirishaji wa dawa za kulevya katika ukanda wa Afrika Mashariki na Ukanda wa Nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara.

Katika hatua nyingine Soko ametoa rai kwa Serikali kuanzisha mazungumzo ya Kidiplomasia na nchi ambazo tayari zimetoa hukumu mbalimbali ikiwemo kifo kwa watanzania ambao wamekamatwa na kesi za dawa za kulevya ili wafungwa hao watumikie vufungo vyao katika nchi yao ya Tanzania.
Waandishi wa Habari.
Hata hivyo amebainisha kuwa mapambano ya dawa za kulevya hapa nchini hayawezi kuzaa matunda kwa kuwa sheria za hapa nchini hazina meno makali ambayo yanaweza kutoa adhabu kali kwa watu wanaokamatwa wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya hali ambayo inasababisha biashara hiyo kuendelea kushamili hapa nchini huku ikiendelea kuliangamiza Taifa kutokana na matumizi ya dawa za kulevya pia kukua kwa kasi kubwa hapa nchini.

"Tunaiomba Serikali ipeleke Mswada wa dawa za kulevya bungeni ili sheria kali ya dawa za kulevya ipatikane jambo ambalo litasaidia katika mapambano dhini ya biashara uingizaji, Usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya hapa nchini" Alisema Soko.

Siku ya Kupinga dawa za kulevya duniani itaadhimishwa kesho ambapo Kitaifa itaadhimishwa katika Mkoa wa Mbea na Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, huku Katika Mkoa wa Mwanza maadhimisho hayo yakitarajiwa kufanyika katika Uwanja mkongwe wa Nyamagana. Kauli mbiu mwaka huu inasema "Uteja wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika, Chukua hatua".
Waandishi wa Habari.
Waandisji wa Habari wakiwa katika Ofisi za OJADACT.

No comments:

Powered by Blogger.