JESHI LA POLISI TANZANIA LAKABIDHIWA MASHINE ZA KUWEKA ALAMA SILAHA.
Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha
kushughulikia Silaha Ndogondogo (RESCA), Bw. Theoneste Mutsindashyaka (kulia)
akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini
Malemi, mashine mbili za kuweka alama silaha, zilizotolewa na Serikali ya
Marekani kupitia Kituo hicho chenye Makao Makuu yake Jijini Nairobi. Hafla hii ilifanyika katika Makao Makuu ya
Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.
Na:Akida Akida
Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha
kushughulikia Silaha Ndogondogo (RESCA), Bw. Theoneste Mutsindashyaka (kulia)
akitoa maelezo jinsi mashine za kuweka
alama silaha zinavyofanya kazi. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, Ernest Mangu.
Mashine za kuweka alama silaha, zilizotolewa
na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania. Uwekaji wa alama katika silaha utasaidia udhibiti
wa matumizi ya silaha hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mwamini Malemi akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhe. Mathias Chikawe kushukuru msaada wa mashine zilizotolewa na Serikali
ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania kwa ajili ya kuweka alama silaha.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IJP Ernest
Mangu akishukuru kuhusu msaada wa mashine za kuweka alama silaha zilizotolewa
na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania katika hafla iliyofanyika
Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam. Waliokaa toka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na Katibu Mtendaji wa Kituo
cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo, Bw. Theoneste Mutsindashyaka.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mwamini Malemi (wa nne kutoka kulia mstari wa mbele) akiwa katika
picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IJP Ernest Mangu (wa tatu toka
kulia) na Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo
(RECSA) Bw. Theoneste Mutsindashyaka (wa nne toka kushoto) baada ya hafla ya
kupokea mashine za kuweka alama silaha iliyofanyika katika Makao Makuu ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wengine ni Viongozi wa Jeshi la Polisi Makao
Makuu na wageni wengine waalikwa.
No comments: