MKUU WA WILAYA YA TARIME AOMBA USHIRIKIANO WA WADAU KUMALIZA TATIZO LA UKEKETAJI WILAYANI HUMO.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Glorious Luoga (anayeongea) amewataka wadau wote kutoa ushirikiano wa kutosha ili kumaliza tatizo la ukeketaji katika wilaya hiyo na kuelekeza nguvu zao zote katika masuala ya maendeleo.
Luoga alitoa wito huo jana wakati akizungumza katika mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) kwa ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society.
“Kila mmoja akitimiza wajibu wake tutamaliza ukeketaji Tarime“, alisisitiza Luoga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la CDF, Koshuma Mtengeti, alitumia fursa hiyo kutambulisha mradi mpya ambao unalenga kuimarisha ulinzi wa mtoto wa kike katika kata tatu za Wilaya ya Tarime ambazo ni Turwa, Bomani na Nyamisangura.
Mradi huo wa miaka mitatu unafadhiliwa na shirika la The Foundation for Civil Society.
Baadhi ya washiriki wa mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF)

Imeandaliwa na Mtandao wa Mara Online
No comments: