LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI MKUU MGENI RASMI UZINDUZI WA MELI MPYA YA MV. NEW MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuzindua meli mpya MV. New Mwanza katika hafla itakayofanyika Alhamisi Januari 23, 2025 eneo la Bandari ya Mwanza Kusini.

Uzinduzi huo umethibitishwa na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Prof. Mbarawa amesema meli ya MV. New Mwanza imejengwa na Mkandarasi Gas Entec Ship- Building kutoka Korea kwa kushirikiana na kampuni ya Meli nchini (TASHICO) kwa gharama ya shilingi Bilioni 120.56.
Amebainisha kuwa hadi sasa meli hiyo imefanyiwa safari sita za majaribio kati ya Mwanza na Bukoba ambazo zilianza kuanzia mwezi Machi 2025 ambapo majaribio hayo yameonesha ufanisi mkubwa uliowezesha wataalamu kuruhusu kuanza kutoa huduma.

Prof. Mbarawa ameongeza kuwa meli hiyo yenye ukubwa wa umbo sawa ghorofa nne itakuwa kubwa zaidi katika ukanda wa maziwa makuu na ina uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari madogo 20 na magari makubwa matatu kwa wakati mmoja.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amewakaribisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo kuanzia majira ya saa mbili asubuhi ambapo mgeni rasmi Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba pia atakuwa na ziara ya kukagua wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kuratibu ufuatiliaji na uokozi katika ukanda wa ziwa Victoria uliopo wilayani Ilemela.

Aeongeza kuwa pia Dkt. Nchemba kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa matenki, vituo vya kusukuma maji na mabomba makuu yamradi wa maji Butimba katika Mtaa wa Sahwa, Kata ya Lwahnima jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.