LIVE STREAM ADS

Header Ads

USHINDI WA CCM ULIOPATIKANA KATIKA MAJIMBO MATATU YA WILAYANI KAHAMA NI “UTATU MTAKATIFU”.

Na:Shaban Njia
Mbunge Mteule katika Jimbo la Msalala lililopo Wilaya Kahama Mkoani Shinyanga Ezekiel Maige amesema kuwa ushindi walioupata wagombea wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Majimbo matatu wilayani humo ni Utatu Mtakatifu ambao utaongeza kasi ya maendeleo ya haraka.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi  wa jimbo hilo Maige alisema kuwa awali maendeleo yalishindikana kupatikana kutokana na kutokuwepo kwa ushirikiano wa kutosha baaina ya mbunge wa awali wa jimbo la Kahama James Lembel, hivyo kwa sasa anaamini kuwa waliochaguliwa watashirikiana na kuwaletea maendeleo wananchi.

Maige alisema kuwa Kahama imeshindwa kupata maendeleo kwa muda mrefu kutokana na mbunge yalikuwepo kutoshirikiana vema na wananchi wake na kuongeza kuwa amekuwa mtu wa kuleta vurugu Bungeni na kukosana na viongozi wa kitaifa,Kimkoa pamoja na kiwilaya jambo ambalo wanakahama wameamua kufanya badadiliko na kumuweka Kishimba.

“Kwanza nina furaha sana baada ya CCM kuchukua majimbo yote matatu ya wilaya ya Kahama, Jimbo la Kahama mjini ambalo lipo chini ya Jumanne Kishimba na Ushetu na chini ya Elias Kwandikwa ambapo nawasihi wananchi kuifanya siku ya oktoba 25 kila mwaka kuwa ya maadhimisho kama ishara ya ukombozi kwao”. alisema Maige.

Kwa uapende wake Mbunge mteule wa jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa, alisema baada ya kumalizika kwa uchaguzi wananchokisubiria ni kuanza kuwatumikia wananchi baada ya kuapishwa hivyon wananchi wa majimbo yote matatu wasubuli maendeleo.

“Tumeanza kufanya kazi baada ya kutangazwa kuwa washindi katika majmbo yote matatu,ambapo namsifu Kishimba kwa kutoa Million 20 katika hospitali ya Kahama mjini pamoja na kutoa vitanda katika wodi ya akinamama wajawazito,hivyo nikuonesha wazi tunaweza kufanya kazi bila kutegemea bajeti ya serikali”. Alisema Kwandikwa.

Aidha Kwandikwa alisema jimbo lake linarasilimali nyingi ambazo zitakuwa fursa kwa wananchi wake kujipatia maendeleo na hivyo kuinua uchumi kwa haraka na kuongeza kuwa wananchi wa ushetu wategemea mabadiliko ya haraka.

“Nitashirikiana na wananchi wangu katika rasilimali zilizopo katika jimbo langu ikiwa ni pamoja na kujenga zahanati ili kupunguza wingi wawagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama,kujenga mabweni katikam shule zote za sekondali ili kupunguza utoro wa wanafunzi sambamba za kupunguza mimba zisizotarajiwa kwa wanafunzi wa kike”. Aliongeza Kwandikwa.

No comments:

Powered by Blogger.