LIVE STREAM ADS

Header Ads

JESHI LA ZIMAMOTO KANDA YA ZIWA LAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA.

Na:Shaban Njia
JESHI la Zimamoto na uokozi Kanda ya Ziwa limeiomba Serikali kuongeza Vitendea kazi kwa Jeshi hilo katika mikoa sita iliyopo katika eneo hilo  pamoja na Ujenzi wa Vituo vipya vya Zimamoto ili kuimarisha utendaji wa kazi  katika mikoa hiyo.

Hayo yalisemwa juzi na Kamishna Msaidizi wa Jeshi kutoka Mkoa wa Mara Endrew Mbate katika kikao kilichowajumisha viongozi mbalimbali wa Jeshi hilo kutoka mikoa sita ya Kanda ziwa  kwa lengo la kubadilishana  mawazo pamoja na kuangalia matatizo yanayolikumba.

Mbate alisema kuwa kikao hicho kilijumusha Mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita pamoja na Mkoa wa Kagera huku wakiangalia mapungufu mbalimbali yanayolikumba Jeshi hili ikiwa sambamba na upungufu wa Vitendea kazi pamoja na kuwa vituo vichache vya zimamoto katika mikoa hiyo.

Aidha Mbate ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho alisema kuwa katika kanda ya ziwa pia kuna upungufu wa watumishi wa Jeshi la zimamoto angawa sio kwa kiasi kikubwa na kuongeza kuwa tayari jeshi hilo limeishaanza kupata Watumishi wapya kutoka makao makuu tangu mwaka jana.

“Upungufu wa Watumishi wa Jeshi la zimamoto kwa kanda ziwa lipo lakini sio kwa kiwango cha juu na tayari jeshi hilo limekwisha pata Watumishi wapya kutoka makao makuu tangu mwaka jana hali ambayo imefanya tatizo hilo kupungua kwa kiasi fulani”, Alisema Endrew Mbate.

Aidha akizungumzia kuhusu vitendea kazi katika Jeshi hilo, Alisema kuwa baadhi ya mikoa imekuwa haina kama vile Mkoa wa Simiyu na Geita ambayo haina Magari ya zimamoto hali inayofanya kazi kuwa ngumu pindi matukio ya moto yanapotokea.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la zimamoto Mkoa wa Shinyanga Elisa Mugisha alisema kuwa kikoa hicho walichokifanya ni mwendelezo wa  vikao vingine na kuongeza kuwa kwa mwezi huu wameamua kukifanyia kikao cho katika Mji wa Kahama kwa lengo pia la kubadilisha mazingira.

Pia alisema kuwa vikao vyao hivyo pia vinajumuisha Wadau mbalimbali wa Jeshi hilo na pia kujifunza kila Mkoa mazingira wanayofanyia kazi na baadaye kuyapeleka makao makuu kwa lengo la kufanyiwa kazi na kupatiwa ufumbuzi kwa haraka.

Alisema kuwa kwa Wilaya ya Kahama kumekuwa changamoto kubwa kwa Jeshi hilo ikiwa ni kukua kwa haraka kwa mji huo huku gari la zimamoto likiwa ni moja na huku jeshi hilo likiwa halina ofisi ya kueleweka kwani ilipo kwa sasa imebanana na ofsi za Halmashauri zilizopo karibu.

No comments:

Powered by Blogger.