LIVE STREAM ADS

Header Ads

MMOJA WA WAHANGA MACHIMBO YA NYANGARATA MKOANI SHINYANGA AFARIKI DUNIA.

Na:Shaban Njia
MMOJA wa Majeruhi watano waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama  kutokana na kufukiwa na kifusi cha Mchanga katika mgodi wa Nyangarata Mkoani Shinyanga na kukaa siku 41 kabla ya kuokolewa aitwae Onyiwa Kaiwao (55) amefariki dunia.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Dr.Joseph Ngowi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa chanzo cha mauti hayo ni kutokana na marehemu kutapika akiwa amelala hali ambayo ilifanya  matapishi hayo kuingia katika njia ya hewa.

“Jana tuliwachukua vipimo Wahanga wote watano na kuonyesha kuwa hali zao ni nzuri lakini Onyiwa alionyesha kutokuwa na maendeleo mazuri tofauti na wenzake na ghafla akiwa amelala alijitapikia hali ambayo matapishi hayo yaliingia katika mirija ya hewa na kuziba hali iliyoababisha kifo chake”. Alisema Dr.Ngowi.

Dr.Ngowi alisema kuwa hali za Wahanga wengine wanne zinaendelea vizuri na kuongeza kuwa wanaendelea na mazoezi huku wakila wenyewe hali ambayo tumepanga kwa siku ya kesho kuangalia uwezekano wa kuwafanyia vipimo kwa mara nyingine tena.

No comments:

Powered by Blogger.