LIVE STREAM ADS

Header Ads

SKAUTI MKOANI SHINYANGA WAMLILIA RAIS MAGUFURI.

Raid Dkt.John Pombe Magufuli
Na:Shaban Njia
Chama cha Skauti Mkoa wa Shinyanga kimemuomba Rais Dkt.John Magufuli kuziagiza Halmashauri hapa nchini kuhakikisha mafungu ya fedha yanatengwa kwa ajili ya shughuli za chama hicho.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa chama cha skauti Wilaya ya Kahama, Fatuma Simba katika semina ya mafunzo ya nishani juu ya uongozi wa skauti, iliyojumuisha viongozi 35 wa skauti iliyofanyika mjini hapa.

Simba alisema kuwa kutokana na ukosefu wa fedha pamoja na kutokuwa na miradi mbalimbali ya kukabiliana na changamoto ndogondogo, baadhi ya vijana hao wameshindwa kufanya shughuli zao kitendo kinachosababisha kundi hilo kupungua kila kukicha.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo, Kamishina wa chama cha Skauti Mkoa wa Shinyanga Mussa Chama, alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo vijana kujiamini, kujitambua na nidhamu kwa watu wa rika zote ama viongozi wao.

Afisa michezo kutoka Halmashauri ya mji wa Kahama Lupola Mkomwa, alisema kutokana na Raisi kuwa mlezi wa Skauti nchini anapaswa kusimamia uboreshaji wa maslahi ya chama hicho.

No comments:

Powered by Blogger.