LIVE STREAM ADS

Header Ads

ACACIA YASOMESHA ZAIDI YA VIJANA 21 CHUO CHA VETA MOSHI MKOANI KILIMANJARO.

Na:Shaban Njia
ZAIDI ya wananchi 21 wanaoishi vijiji jirani na Mgodi wa Bulyanhulu wamehitimu mafunzo ya fani mbalimbali za uchomeleaji vyuma, ufundi waya wa umeme wa magari katika chuo cha ufundi (VETA) Moshi chini ya ufadhili wa Kampuni ya ACACIA kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu.

Hayo aliyasema jana msimamizi wa mradi wa IMTT. Mathias Kalulu katika hafra fupi ya kuwaaga wahitimu hao iliyofanyika mgodini hapo na kusema kuwa licha ya vijana 21 kuhitimu mafunzo hayo lakini kuna vijana wengine 68 wanaendelea na mafunzo hayo chuoni hapo.

Kalulu alisema kuwa mradi huo umelenga kusomesha vijana wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka mgodi huo ambao walihitimu masomo yao ya kidato cha nne na kushindwa kujiendeleza kielimu.

“Mradi wa IMTT  umelenga kusaidia kusomesha vijana waliohitimu masomo yao ya kidato cha nne na kushindwa  kujiendeleza kielimu hasa hawa wanaoishi vijiji jirani zaidi na mgodi huo kwa kuwasomesha ili wajiajiri wenyewe hapo baadaye”,alisema Kalulu msimamizi wa mradi.

Aidha Meneja huyo alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa mradi wa IMTT kutoka 2009 hadi sasa, ni kundi la sita la vijana wapatao 147 wanaoishi katika vijiji hivyo vinavyozunguka mgodi huo wamewezeshwa ambapo ukiondoa idadi ya vijana 68 wanaoendelea na masomo chuoni hapo.

“Vijana waliomaliza kidato cha nne na kushindwa kujiendeleza kielimu kampuni ya Acacia kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu uliamua kuwafadhili kwa kuwasomesha katika chuo cha VETA ili wapate mafunzo ya ufundi umeme wa majumbani,umeme wa magari (Wireling) pamoja na uchomeleaji wa vyuma huko Moshi lengo la mgodi ni waimarike na baadaye waweze kujiajiri na baadaye kupata ajira mgodini,”aliongeza Kalulu.

Hata hivyo Kalulu alisema kuwa wanafunzi hao kipindi wanapokuwa likizo wanarudi mgodini kwaajili ya kufanya mazoezi ya vitendo badala ya kumaliza likizo yao wakiwa nyumbani nakuongeza kuwa kufanya hivyo lengo la mgodi ni vijana hao kuwa wazoefu kipindi wanaporudi masomoni.

Akizungumza mmoja wa vijana waliohitimu mafunzo hayo Kumba Matory mkazi wa kijiji cha Bushing’we Kata ya Bulyanhulu alisema kuwa wanaushukuru uongozi wa mgodi huo kwa kuwapa elimu hiyo kwani kwa sasa wanaweza kuyamudu maisha kwa kuwa wanauhakika wa kufanya kazi kwa kutumia elimu hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.