LIVE STREAM ADS

Header Ads

ALLIANCE SPORTS ACADEMY KUTOKA JIJINI MWANZA WAIBUKIA MBULU MKOANI MANYARA.

NA OSCAR MIHAYO, Mwanza
Timu ya Alliance Sports Academy ya  Jijini Mwanza inayoshiriki ligi daraja la pili,  imeondoka jana kwenda Mbulu Mkoani Manyara ikiwa na viongozi wanane na wachezaji 20 tayari kwa ajili ya mechi ya ligi hiyo itayotachezwa kesho.

Kocha msaidizi wa timu hiyo Matias Wandiba alisema kuwa vijana wako kwenye hali nzuri ya kushinda mchezo huyo na kuongeza kuwa kwao kila mechi ni fainali.

“Sisi kama alliance tunawahaidi wanamwanza kuwa kila mechi kwetu nia Fainali hivyo wapenzi na mashabiki wategemee matokeo mazuri kwani timu haina majeruhi yoyote”.Alisema Wandiba.

Alliance iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikilingana pointi na timu ya Bulyankulu kutoka mjini Shinyanga huku ikizidiwa goli moja ikiwa na magoli manane na kufungwa matatu huku wenzao wakiwa na magoli tisa wakiwa wamefungwa magoli matatu.

No comments:

Powered by Blogger.