ELIMU BURE YAZUA KIZAA ZAA KWA WAZAZI WA WANAFUNZI WANAOSOMA ELIMU YA WATU WAZIMA MKOANI MWANZA.
Baadhi
ya Wazazi wa Wanafunzi wanaosoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari
Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, leo wameandamana hadi
katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ili kufikisha kilio chao, baada ya
kubaini kwamba watoto wao wanasoma elimu ya watu wazima shuleni hapo tofauti na
mategemeo yao.
Wakizungumza nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, wazazi hao wamesema kuwa miaka miwili ilioyopita waliwaandikisha watoto
wao katika shule hiyo kwa ajili ya kuanza masomo ya kidato cha kwanza, lakini
wamepigwa butwaa baada ya kubainika kuwa watoto wao walijumuishwa katika
kitengo cha elimu ya watu wazima kutokana na ufaulu waliokuwa nao ambao ni
chini ya wastani wa pointi mia (100).
Wamesema wameyabaini hao baada ya watoto wao
kurudishwa nyumbani baada ya kuwa hawajalipa ada ya mhula wa masomo wa mwaka
huu, wakati Serikali imepitisha mpango wa elimu bure nchini, na kwamba baada ya
kufuatilia suala hilo ndipo waliambiwa kwamba watoto wao hawako katika mpango
huo wa elimu bure kwa kuwa wao wako katika mpango wa elimu ya watu wazima ambao
wanafunzi wake wanalipa ada kama kawaida.
Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari
katika Manispaa ya Ilemela, amekanusha madai ya wazazi hao kuwa hawakujua kama
watoto wao wanasoma elimu ya watu wazima na kuongeza kuwa wazazi hao wameamua
kuandamana hadi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza baada ya kubaini wanafunzi
wa elimu ya Watu Wazima wanapaswa kulipa ada na si kusoma bure.
Amesema elimu zaidi inaendelea kutolewa kwa wazazi
kuhusiana na mpango wa elimu bure ulioidhinishwa na Serikali ya awamu ya tano
chini yake mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli ili kuondoa mikanganyiko mbalimbali
inayojitokeza.
Mmoja wa wazazi walioandamana akitoa ufafanuzi kwa wenzake
Mmoja wa wazazi walioandamana akitoa malalamiko yake kwa wanahabari
Baadhi ya Wazazi walioandamana
Nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Kutoka Viunga vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mimi ni GB Pazzo wa Binagi Media Group (Kulia).
Soma Kilichofuata HAPA
No comments: