LIVE STREAM ADS

Header Ads

HALI TETE SOKO LA NYAHANGA KAHAMA MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Tatizo la ukosefu wa choo katika Soko la Nyahanga katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, bado ni changamoto kubwa ambayo imeshindwa kutatuliwa hali inayowatia hofu wafanyabiashara kufungwa kwa soko hilo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyahanga lilipo Soko hilo, Supa Said (CHADEMA) amesema tatizo la ukosefu wa choo katika soko hilo, ni la muda mrefu na kwamba ofisi yake itaendelea kuhimiza kujengwa choo hicho.

“Kimsingi kero hii ipo tangu uchaguzi haujaanza na wafanyabiashara wamelalamika hadi wamechoka, niwaahidi wafanyabiashara kuwa kero hii nitahakikisha inafikia ukomo, Nyahanga ina vyanzo vingi vya mapato, kuna milima ambayo tunaweza kupasua mawe, pia tuna wawekezaji wengi katika Kata yetu hali ambayo ingesaidia kutatua kero hiyo”. anasema Said.

Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Amiri Yusuph amesema kuwa amelazimika kuazima choo cha muda katika Kanisa la Wasabato lililopo jilani na ofisi hiyo kwa ajili ya watumishi wake kutumia kwa muda huku akilipa kodi ya shilingi elfu kumi (10,000) kila mwezi, wakati ofisi yake ikijipanga kuhakikisha  ujenzi wa choo unaanza.

Nae Diwani wa Kata ya Nyahanga Michael Magile amesema kuwa iwapo wataalamu wa Afya watalifunga soko hilo ni vyema wakaanza kuifunga kwanza ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo kwani nayo haina choo jambo ambalo ni uzembe wa mtendaji.

Suala la kosefu wa vyoo katika Kata Soko hilo, kiafya inahatarisha hali ya usalama wa wafanyabiashara wa soko hilo pamoja na wateja wao ikiwemo kuwa katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya kuhara kama vile kipindupindu.

No comments:

Powered by Blogger.