LIVE STREAM ADS

Header Ads

KISHIMBA ASAIDIA WODI YA WAZAZI MJINI KAHAMA. ATOA VIFAA VYA KUJIFUNGULIA.

Na:Shaban Njia
KATIKA kuhakikisha kuwa Wajawazito katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama wanajifungua salama Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba ametoa Vifaa maalumu kwa ajili ya kujifungulia (birthing kit) vyenye thamani ya shilingi milioni  tano ili kufanikisha mpango huo.

Akimkabidhi vifaa hivyo kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama Bruno Minja Mbunge huyo alisema kuwa ameamua kundelea kusaidia Hospitali ili kuhakikisha kuwa hakuna matatizo yeyote anayopata mama mjamzito katika harakati za kujifungua.

Kishimba ambaye pia alikagua matatizo mbalimbali yanayoikabili Hospitali hiyo alisema kuwa msaada huo ni mwendelezo wa misaada mbalimbali ikiwa moja ya ahadi zake alizozihaidi katika kampeni zake za ubunge katika kuhakikisha kuwa huduma za afya zinaimarika kwa kiwango kikubwa katika Hospitali hiyo.

Alisema kuwa Hospitali ya Wilaya ya Kahama inakabiliwa na Changamoto nyingi ikiwa pamoja na upungufu mkubwa wa dawa za wagonjwa kisukari hali ambayo inahitajika jitihada kubwa katika kuhakikisha kuwa tatizo hilo linakwisha kwa haraka hali ambayo itapunguza usumbufu uliopo kwa sasa kwa Wagonjwa wa ugonjwa huo kwa sasa.

“Ninajua Hospitali hii ina changamoto nyingi kwani kwa sasa inatoa huduma kwa Wilaya zilizopo katika Mikao jirani hali ambayo inafanya wakazi wa Wilaya ya Kahama kukosa huduma stahiki ikiwa ni pamoja na upungufu mkubwa wa dawa hususani zile za magonjwa ya Kisukari.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Bruno Minja alisema kuwa anapata changamoto nyingi kutokana na kuhudumia wagonjwa wengi hususani wale wanatoka katika Wilaya jirani kama vile za Ny’angwale, Urambo Bukombe, Geita pamoja na Wilaya mpya ya Kaliuwa.

Alisema kuwa kumekuwa na upungufu mkubwa wa dawa kutoka na dawa nyingi zinazokuja zinaenda katika makundi maalumu ikiwa ni makundi ya wazee, Watoto wenye umri chini ya miaka mitano, akinamama wajawazito , wagonjwa wa kifua kikuu , Ukimwi pamoja na Wagonjwa wenye kisukari hali ambayo inafanya bajeti ya Hospitali kutokukidhi Wananchi.

Pia Mganga Mkuu huyo alisema kuwa Hospitali hiyo ina upungufu wa  magari hali ambayo inawia vigumu kufika Vijijini katika harakati za kutoa mchanjo kwa akinamama Wajawazito pamoja na watoto huku akisema kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha pungufu tofauti na bajeti wanayoipanga katika Hospitali hiyo.

Alisema kuwa Hospitali yake imekuwa ikihudumia wagonjwa wengi kuliko Hospitali ya Mkoa ambapo katika bajeti ya nusu waliomba fedha shilingi milioni 600 kukidhi mahitaji ya uendeshaji wa Hospitali hiyo lakini walipewa shilingi milioni 280 hata hivyo mpaka kufikia sasa fedha hizo hazijafika hali ambayo Halmashauri ya Mji aemeamua kubeba jukumu hilo la kununua dawa hizo.

No comments:

Powered by Blogger.