SERIKALI YATOA ONYO KWA WATENDAJI WANAOKULA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO.
Na:Shaban Njia
SERIKALI Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga imewaonya Watendaji wa Halmashari Wilayani hapa kuacha kujihusisha na ufujaji wa fedha za Wananchi zinazotolewa wawekezaji kwa ajili ya shughuli za Maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa alitoa onyo hilo wiki hii wakati akizunguza na waandishi wa Habari ofisi kwake na kutoa ufafanuzi juu ya fedha za ushuru wa huduma zilizotolewa na Mgoagi wa Dhahabu wa Acacia Buzwagi kwa Halmashauri ya Mji wa Kahama kuhujumiwa na baadhi ya Watenadji wake.
Kawawa alisema kuwa kwa sasa ameamua kuanza na Halmashauri ya Mji wa Kahama na baadaye atahamia katika Halmashauri ya Msalala ambapo kuna Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kama kutakuwa na matatizo kama hayo.
Alisema kuwa kwa sasa lazima wafanyakazi wa Serikali wafanye kazi kwa kufuata weledi na nidhamu kazini hali ambayo itainua utendaji wao wa kazi na Wananchi kunufanika na wawekezaji waliopo katika maeneo yao na Wilaya ya Kahama kwa ujumla.
Kwa Serikali iliona ianaze kwanza na Halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo kengele ndio ilikuwa ikilia zaidi tofauti na Halmshauri nyingine lakini ukiona mwezio nanyolewa ni bora na wewe ukaanza kutia maji kwani kwa sasa Serikali ya awamu ya tano haina mchezo na uchezaji wa fedha za Wananchi”, Alisema Vita Kawawa.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa katika ripoti yake ya uchunguzi aliyoisoma katika Baraza la Halmashauri ya Mji wa Kahama hivi karibuni pia tayari ameisha tuma orodha ya makapuni feki katika ngazi husika yalijihusisha katika ukandarasi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Pia aliendelea kusema kitendo cha Makampuni 151 katika Mgodi wa Buzwadi kutilipa fedha hizo za ushuru wa huduma ni uzembea wa Halmashauri husika kwani Mgodi huo ulitenga ofisi kwa ajili ya Watumishi wa Halmashuri kuja ufanya tathimini ya Ushuru wanaoupata kwa mwaka kutokana na makampuni hayo.
Hata hivyo alisema kuwa hata hayo makapuni 17 yaliokuwa yamelipa kodi, yalikuwea yakilipa kidogokidogo hali ambayo imeifanya halmshauri hiyo kutofikia malengo ya ukusanyaji huo na kufanya baadhi ya miradi mbalimbali ya maendeleo kutokamilika kabisa.
Hivi karibuni Halmashauri ya Mji wa Kahama iliwasimamisha kazi watumishi wake watano kwa tuhuma za matumizi mabaya fedha za Ushuru wa Huduma kiasi cha shilingi milioni 400 zilizokuwa zimetolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kwa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kumalizia miradi mbalimbali ya maendeleo.
No comments: