LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC SHINYANGA AAGIZA WAHAMIAJI HARAMU WANAOFANYA KAZI KATIKA MASHAMBA YA TUMBAKU KUCHUKULIWA HATUA

Na Shaban Njia, Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ameitaka Idara ya Uhamiaji Wilayani hapa kuhakikisha kuwa inawakamatwa wahamiaji haramu kutoka katika nchi jirani wanaokuja kufanya kazi katika mashamba makubwa ya Tumbaku.

Rufunga alisema hayo wakati akizungumza na Watendaji katika Halmashauri ya Mji wa Kahama ikiwa ni sambamba na Kamati ya Ulinzi na Usalama katika ziara yake ya kawaida ya kukagua shughuli za maendeleo katika Halmashauri hiyo ya Mji.

Alisema kuwa kuna baadhi ya makundi makubwa ya Wahamiaji haramu kutoka katika baadhi ya nchi jirani za Burundi na Rwanda wanaotumiwa na wakulima wa Tumbaku katika kata mmbalimbali hususani ya Ulowa ambapo ndipo inalimwa kwa  wingi.

“Kuna Mkulima wa Tumbaku anayeitwa Safari Manjala ana jumla ya Wahamiaji haramu zaidi ya hamsini wanaofanya kazi katika mashamba yake ya tumbaku bila ya kuwa vibali maalumu vya kuishi nchini lazima watu hawa wafuatiliwe ili kujua uhalali wao wa kuishi nchini” alisema Rugunga.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliendelea kusema kuwa kutokana na baadhi ya nchi jirani kuwa na dalili za machafuko nanyingine tayari yakiwa yameanza ni vema kulinda mipaka yetu na kutowahifadhi watu kama hao katika maeneo yetu tunayoishi.

Hata hivyo Rufunga alisema kuwa kwa sasa idara ya Uhamiaji ya Wilaya ya Kahama na Mkoa mzima wa Shinyanga kuhakikisha kuwa watu hao hawaiingii nchini bila ya vibali maalumu kutoka uhamiaji kwani kwa kufanya hivyo kutaapunguza wimbi la Wahamaji hao kuingia hapa nchini.

Kwa upande wake Safari Manjala anayetuhumiwa kuwahifadhi wahamaiaji hao ikiwa ni pamoja na kuwapa ajira kwa ujira mdogo katika mashamba yake ya Tumbaku alisema kuwa yeye kwa sasa hawatumii watu hao katika kilimo cha tumbaku bali amekuwa akiwatumia wananchi katika kata hiyo.

“Mimi kwa sasa ndugu Mwanaadishi wa habari siwatumii wahamiaji hao katika shughuli zangu za Kilimo cha Tumbaku katika kata ya Ulowa bali kuna watu wanaokuja kutoka katika maeneo mbalimbali katani kwangu kutafuta ajira katika mashamba yangu.

Hata hivyo Manjala akili kwakuwatumia warundi hao kwakipindi cha nyumba ambapo alisema kuwa baada ya ofisi ya uhamiaji wilaya pamoja na mkoani kufanya upresheni kimbunga katika baadhi ya mashamba ya tumbaku kwakuogopa kukamatwa aliwarudisha nchini mwao.

Wakulima wa Tumbaku katika Kata ya Ulowa amabyo ni maarufu kwa kilimo hicho Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamekuwa wakiwahifadhi wahamiaji haramu kwa kuwapa ajira kwa ujira mdogo au kwa kuwapa chakula tu hali ambayo imefanya kuwepo kwa makundi makubwa yanayoenda kufanya jkazi hizo katika maeneo hayo kwa wingi.

No comments:

Powered by Blogger.