LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATENDAJI WABANWA KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
WATENDAJI wa Vijiji katika kata zilizopo katika Halmashauri za Msalala, Ushetu pamoja na Mji katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Watendaji wa Kata katika kuhakikisha kuwa Wanafunzi 705 ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza katika sekondari za Serikali katika Halmashauri zao wanaanza masomo mara moja.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kwawa aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya siku moja ya kutembelea Halmashuri hizo  kuona shughuli za utengenezaji wa Madawati zilizopofikia na kuhakikisha kuwa hadi ifikapo mei 15 zoezi hilo liwe limekamilika.

Kawawa alisema kuwa kwa sasa lazima Watendaji wa Vijiji watoa ushirikiano mkubwakwa wale wa kata ili kuhakikisha kuwa kundi hilo la Wanafunzi ambalo hadi kufikia hivi sasa bado halijaripoti katika Shule za Sekondari za Serikali walizopangiwa kwenda kusomea.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama aliendelea kusema kuwa idadi ya Wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza imekuwa ni kubwa huku baadhi shule za Sekondari za Serikali zikibaki kuwa na mrundikano mkubwa wa Wanafunzi hali inayopelekea kuwepo na upungufu mkubwa wa Madawati.

“Ninawaagiza Watendaji wa Vijiji kutoa ushirikiano kwa wale wenzenu katika kuwatafuta Wananfuzi hao ambao hawajaripoti Madarasani hadi kufikia sasa kwani nyinyi ndio mpo karibu na Kaya zenye Wanafunzi hao na mzazi atakagoma kumpeleka Mwanae kuanza shule basi sheria itachukua mkondo wake kwa Mzazi husika”, Alisema Vita Kawawa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Watendaji wa Halmashauri hizo tatu kuhakikisha hadi kufikia mwezi mei shule zote msingi zilizopo katika Halmashauri zao zinaondokana na tatizo la upungufu wa Madawati.

Akiongea na Wakurungenzi wa Halmashauri hizo kwa nyakati zofauti Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama aliwataka viongozi kuhakikisha wanamaliza tatizo hilo kwani liimekuwa ni kero katika Shule za Msingi pamoja na Wazazi katika kuitikia sera ya Elimu bure iliyotolewa na Rais wa awamu ya Tano Dr, John Pombe Magufuli.

Alisema kuwa kufuatia Sera hiyo ya Elimu bure wazazi wamejitokeza kwa Wingi kuandikisha watoto wao darasa la kwanza huku wakikutana na Changamoto ya shule kuzidiwa na Wanafunzi hali ambayo imechagia kuwepo kwa upungufu mkubwa wa Madawati katika shuile hizo.

“Tumehangaika kutafuta mbao kwa ajili ya ujenzi wa Madawati kumaliza tatizo kuanzia hapa Kahama hadi nje ya Wilaya hii na kuonekana kuwa tatizo ndio limekuwa changamoto kubwa katika kuharakisha utengenezaji wa Madawati hayo na kuyakabidhi kwa Mkuu wa Wilaya kabla ya kufikia tarehe hiyo”, Alisema Patrick Karangwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala.

No comments:

Powered by Blogger.