LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHANGAMKIA FURSA HII KUTOKA TAASISI YA INTERNATIONAL LANGUAGE TRAINING CENTRE YA JIJINI MWANZA.

Lugha ni njia bora ya Mawasiliano kwa maisha ya kila siku ya Mwanadamu. Ikiwa utaishi katika jamii ambayo huelewi lugha yake basi ni dhahiri, shairi kwamba utakosa fursa nyingi zinazopatikana katika jamii hiyo ikiwemo fursa ya kibiashara.

Ni kutokana na umuhimu huo, Taasisi ya Kufundisha Lugha ya International Language Training Centre inayopatikana Isamilo karibu na Medical Research Jijini Mwanza, imetoa fursa Kwa Watanzania na Wasio Watanzania kujifunza lugha mbalimbali za Kimataifa na Kitaifa ikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kichina, Kijapani, Kiswahili pamoja na lugha za Makabila kwa wageni kama vile Kisukuma.

"Mbali na kufundisha lugha, pia tunatoa mafunzo ya Computer kwa watu wote, huku pia tukitoa elimu ya makuzi kwa watoto wadogo kupitia Day Care Centre tuliyonayo". Anasema Charles Mombeki ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.