LIVE STREAM ADS

Header Ads

DUNIA NZIMA, MACHO NA MASIKIO YAMEANGAZIA UCHAGUZI WA MARUDIO VISIWANI ZANZIBAR.

Wakazi wa Tanzania Visiwani (Zanzibar) hii leo wanapiga kura kuwachagua viongozi wao akiwemo Rais wa Zanzibar baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar uliofanyika Octoba 25 mwaka jana kufutwa.

Uchaguzi huo ulifutwa kutokana na kile kilichoelezwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, Jecha Salim Jecha kuwa ni kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo baadhi ya mawakala wa vyama vya siasa kupigwa na kufukuzwa katika vituo vyao vya kazi.

Uchaguzi huu wa marudio unafanyika huku ukiwa umesusiwa na baadhi ya vyama vya upinzani ikiwemo CUF, kutokana na kutokubaliana na maamuzi ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa awali, jambo ambalo linafanya macho na masikio kote duniani kuuangazia uchaguzi huo.

No comments:

Powered by Blogger.