LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUTANO MKUU WA BODABODA MKOA WA MWANZA WAADHIMIA KUANZISHWA KWA UMOJA WA BODABODA TAIFA.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) akuzungumza katika Mkutano Mkuu Muhura wa Kwanza wa mwaka 2016 wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Mwanza uliofanyika Jumamosi Machi 19,2016 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Pamba Jijini Mwanza. Kushoto kwake ni viongozi wa bodaboda Mkoa wa Mwanza.
Picha na Mdau Wetu!
Katika Mkutano huo, Konisaga ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alitaka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabara kuzidisha juhudi za kutoa elimu ya usalama barabarani ili kupunguza ajali, badala ya kasi iliyopo ya kutoza faini kwa watumiaji wa vyombo vya barabarani.

Mwenyekiti wa bodaboda Mkoa wa Mwanza Makoye  Kayanda amesema "pamoja na Mambo mengine, Wajumbe wa Mkutano huo walikubaliana kwa sauti moja kuanzishwa kwa Umoja wa Bodaboda Taifa ili kurahisisha utatuzi wa Changamoto zinazoikabiri sekta ya usafirishaji abiria ya Bodaboda".

Alisema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kuvamiwa, kutekwa, kuuawa na kuuawa kwa waendesha bodaboda huku bodaboda zao zikiibiwa. Kutafuta suluhu ya baadhi ya watu wakiwemo bodaboda kutumia fursa hiyo katika kujihusisha na uhalifu nchini. Utii wa Sheria bila shuruti pamoja na kujadili namna bodaboda wanavyoweza kushirikiana na taasisi mbalimbali zikiwemo za binafsi na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya sekta hiyo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Viongozi wengine wa Bodaboda kutoka Mikoa ya Mara, Tabora, Singida, Shinyanga, Kilimanjaro pamoja na Viongozi wa sekta nyingine ambazo ni wadau wa usafirishaji ambao ni Machinga, Mamalishe, Daladala, Mabasi, RTO, Sumatra pamoja na TRA.
Wajumbe wa Muungano wa Bodaboda Mkoa wa Mwanza wakiwa katika Mkutano Mkuu uliofanyika Jijini Mwanza jumamosi iliyopita.
Mwenyekiti wa bodaboda Mkoa wa Mwanza Makoye Kayanda (wa tatu kulia) akiwa pamoja na viongozi wengine wa bodaboda katika Mkutano Mkuu wa Bodaboda Mkoani Mwanza uliofanyika Jijini Mwanza jumamosi iliyopita.
Baadhi ya viongozi wa bodaboda waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Bodaboda Mkoani Mwanza uliofanyika Jijini Mwanza jumamosi iliyopita.
Viongozi mbalimbali wa bodaboda wakiwa pamoja na bodaboda katika picha ya pamoja katika Mkutano Mkuu wa Bodaboda Mkoani Mwanza uliofanyika jumamosi Machi 19,2016.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.

No comments:

Powered by Blogger.