LIVE STREAM ADS

Header Ads

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: KATAA UKATILI KWA WASICHANA NA WANAWAKE CHOCHEA USAWA WA KIJINSIA.

Mmoja wa Wanawake nchini akimnyonyesha mwanae baada ya shughuli za uzalishaji.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
March 08, Kila Mwaka Tanzania huungana na Mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani. Mara kadhaa siku hii imekuwa ikitumika kwa ajili ya kupaza sauti zaidi katika kuiasa jamii ili kuondokana na mitizamo hasi juu ya Mwanamke ambayo imekua ikiibua ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Wasichana katika jamii.

Siku hii imekuwa ikitumika kuiambia jamii kwamba ni Ukatili kumnyima mtoto wa kike elimu, ni ukatili kumkeketa Mtoto wa Kike, Ni ukatili mwanamke kutoruhusiwa kumiliki ardhi, ni ukatili mme kumpiga mkewe na matendo mengine mengi miongini mwa hayo.

March 08, 2016 Tanzania ikiwa inaadhimisha Siku hii ya Mwanamke Duniani, ni vyema wananchi wakatambua kwamba kila mmoja (Mke na Mme) wanayo haki sawa katika jamii hivyo tofauti ya kijinsia isiwe chanzo cha mwanamke kutendewa ndivyo sivyo.

Binagi Media Group, kupitia Binagi Blog tunawatakia Maadhimisho Mema ya Siku ya Wanawake Duniani. Kataa Ukatili kwa Wasichana na Wanawake, chochea usawa wa Kijinsia katika jamii.
Soma Zaidi HAPA Kuhusu Siku Hii ya Wanawake Duniani.

No comments:

Powered by Blogger.