LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKA LA MPANGO WA INJILI YA YA UPONYAJI TANZANIA LAANZA KUWANUSURU ALBINO.

Judith Ferdinand, Mwanza
Jamii imeombwa kuachana vitendo vya kikatilii kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), badala yake iwapende, iwajali na kuwasaidia katika masuala mbalimbali ikiwemo ajira ili waweze kujitegemea kiuchumi.


Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  "Mpango wa Injili ya Uponyaji Tanzania", Lucy Haruni, linalojishughulisha na kutetea watu wenye ulemavu wa ngozi, katika tamasha lililofanyika kwenye kanisa la KKKT  Ushirika wa Angaza Igoma mkoani hapa.

Alisema, ili kukomesha mauaji ya walemavu wa ngozi, jamii inatakiwa kuwa rafiki wa kundi hilo kwa ajili ya kuwafuta simanzi walionayo ya kuuwawa na kuachwa na ulemavu.


Aidha alisema, ameamua kufanya matamasha ili aweze kupata fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi itakayowasaidia watu wa kundi hilo kwani mpaka sasa amefanikiwa kupata pikipiki nne za kuanzia, zenye thamani ya sh. milioni 10, ambazo zitatumika kusafirisha abiria na kuwasaidia kujikimu kimaisha.

Kwa upande wake Mwenyekiti CCM wilaya ya Misungwi Judith Mlolwa,  aliyemwakilisha Meya wa jiji la Mwanza James Bwire aliiomba, jamii iache kufanya mauaji kwa watu hao kwani ni binadamu  kama wengine na  wanauwezo wa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo ya maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa  Chama cha Watu wenye Ulemavu wa  Ngozi mkoa wa Mwanza, Alfred Kapole, alisema imetosha kwa vitendo vya mauaji ya albino hivyo asingependa kusikia mambo hayo yakiendelea kwani yanamfedhehesha Mwenyezi Mungu.

No comments:

Powered by Blogger.