LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAHAKAMA KUU NCHINI YAAHIDI USHIRIKIANO KUFANIKISHA UHURU WA HABARI.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba (kulia) akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016.
Na:BMG
Mhe.Makaramba amefungua maadhimisho hayo ambayo Kitaifa yamefanyika Jijini Mwanza, kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Mohamed Chande Othman.

Amesema Mahakama Kuu nchini iko tayari kutoa ushirikiano baina ya pande zote mbili ili kufanikisha kuwepo kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye, wamehudhuria maadhimisho hayo.

Nape amesema Wizara yake inatoa fursa ya kupokea mapendekezo juu ya suala la Urushaji wa Matangazo ya bunge Live (moja kwa moja) pamoja na kuhakikisha Sheria kandamizi kwa Vyombo vya habari ikiwemo sheria ya Magazeti ya Mwaka 1977 zinaondolewa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye akitoa salamu zake katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016.
Dominica Haule kutoka GEMSAT akitoa salamu zake katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016.
Mgeni Rasmi, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba (wa pili kulia) akizindua Chapisho la sera ya Jinsia kwa Vyombo vya Habari vya Kijamii nchini.
Mgeni Rasmi, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba (wa pili kulia) akizindua Chapisho la sera ya Jinsia kwa Vyombo vya Habari vya Kijamii nchini.
Picha ya Pamoja

No comments:

Powered by Blogger.