LIVE STREAM ADS

Header Ads

JICHO LA BMG: RAY C AMESAIDIWA MPAKA NA IKULU, JE ANATAKA MSAADA GANI ZAIDI?

Image result for EMAGE RAY C
Na Pio Pius (Mdau)
Msanii RAY C amesaidiwa mpaka na IKULU lakini amerejea kule Kule, je anahitaji Msaada gani tena Zaidi ya Kumrejea MUNGU?.... Wapo Mateja all around hawajawahi kupata hata Panadol ya Serikali ya Mtaa!

Wapo walio tayari kumchangia akatibiwe lakini je Vipi kuhusu UTAYARI wake?...Maana TIBA yoyote inahitaji Utayari wa Muhusika Otherwise tutajikuta tunachangisha FEDHA za kwenda kulifanyia Massage Gogo la Mnazi.

Huwezi kutia huruma kwenye Macho ya Watu pasipo kujihurumia wewe Mwenyewe!..,. wapo wanaosema anaruka ruka huko Mitaani kama kichaa,...na hii yote ni ADDICTION ya Unga.....pengine Moyo wake unataka, Mwili hautaki, amekuwa Chronic, Je Wasanii wanajifunza nini hapa?....Maana nasikia Mnabwia Unga mpaka mnalala Mashineni badala ya Studio,..what the hell is this, Tunaiga USA?

Kama Taifa ni vema kutibu na kusaidia MATEJA lakini Bado hili sio Suluhisho la Kudumu....Suluhisho ni kushirikiana kutengeneza Jamii au kizazi kisichokuwa na Mateja,....na hii ianzie katika Ngazi ya Familia mpaka Serikali Kuu....Kwa kuanzia na Malezi ya Familia mpaka Sera dhidi ya Madawa Kitaifa.

WASANII wengi Mnakula Unga kimya kimya,..mnatoka Mtokako...mnahangaika na Sanaa...inawalipa....mkipata Vihela mnajaribu kila aina ya Vilevi ambavyo hamjawahi kutumia....mnajaribu umalaya ambao hamjawahi kufanya, eti "We gat Cash hommies lets Show them!".....SHOW WHO? stupid!

Na Mara nyingi ukiona Msanii ameanza kuposti picha za Viatu instagram badala ya Selfie alizozoea tunapata Mashaka na AFYA yake for the time being kama yupo Salama!,.....Tunaendelea Kupoteza Vipaji vingi kila Mara, but sijawahi kusikia hata Siku Moja mmeitana Mahali kujadili Mustakabali wenu Kiafya na Kisanàa.....Nyinyi mnaitana kwenye BATA tu!...bado haieleweki hata kama mna Chama au Umoja wa Kuwaunganisha,...ila ikifikia mmepata Matatizo kwa RAHA zenu hapa Mjini ndio mnataka Mpaka Mkulima wa Ufuta kule Mahenge aje awasaidie....This is SHAME.

Huu ni USHAURI wa Bure kabisa (Tax exempted)..otherwise Msipochukua Hatua Stahiki Mtakwisha wote....atakayebaki ni yule sanamu wa kwenye Mnara wa Askari.....tulimkuta na tutamuacha.

Mwenye Rafiki yake Msanii am-tag kwenye Comment..najua Wasanii wengi wanajitia kichwa cha kondoo, masikio kwenye kwapa na Macho kwenye Unyayo, hawaoni na wala hawasikii, ...But the Right time will tell.

No comments:

Powered by Blogger.