LIVE STREAM ADS

Header Ads

MASANJA KUGOMBEA UWENYEKITI CUF TAIFA.


Na Shaban Njia
Siku chache baada ya kuripotiwa katika vyombo vya habari kuwa Professa Ibrahim Lipumba, atagombea tena Uenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, baadhi ya wanachama wa chama hicho wameanza kujitokeza na kuonesha nia ya kugombea wadhifa huo katika Uchaguzi mkuu ambao bado haujajulikana utafanyika lini ndani ya mwaka huu.

Akiongea na Wandishi wa Habari nyumbani kwake, Koplo Stephen Masanja, ambaye ni Katibu wa CUF wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, alitangaza adhima yake ya kuwania nafasi hiyo kubwa ndani ya chama, kwa mara nyingine baada ya kufanya hivyo mwaka 2009.

Koplo Masanja, alisema ataomba kwa mara ya pili nafasi hiyo baada ya kuthubutu kufanya hivyo kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa mwaka 2009, akiwa na akina Profesa Abdallah Safari na Ibrahim Lipumba, na kufanikiwa kushika nafasi ya pili, akiachwa kwa kura nyingi na Profesa Lipumba, nae akimuacha kwa kura chache Profesa Safari.

“Nia yangu ya kugombea ni kutaka kurudisha chama kwa wanachama wilayani na katika Kata na matawi. Kwa muda mrefu sasa CUF imebaki makao makuu tu. Viongozi wanafanya siasa kwa lap top (komputa mpakato), sasa utampataje mwanachama wa Nkasi na Ushetu, kwa Lap Top?”. Alihoji Koplo Masanja.

Aliongeza kwa kusema, “Nikipewa ridhaa ya kuwa Mwenyekiti nitahakikisha nimefika kila wilaya hapa nchini kwa lengo la kuimarisha chama na kwapa malengo viongozi wa kila wilaya kufika katika Kata,na wa Kata kufika kila Kitongoji.”

Alisema lengo ni kuirudisha CUF ya mwaka 2000 ambapo kila kijiji ilikuwepo kinyume na ilivyo hii leo, ambapo imejikita katika baadhi ya maeneo kwa uchache huku hali hiyomya cham,a kuporomoka inasababishwa na baadhi ya viongozi wa sio kuwa na madili.

Koplo Masanja ni mwanachama mwanzilishi wa chama cha wananchi CUF, chini ya James Mapalala, ambapo alifanikiwa kushika nafasi kadhaa za chama, kabla ya mfumo wa vyama vingi amepata kuwa Katibu Msaidizi wa UVCCM wilaya ya Kahama tangu mwaka 1977 hadi 1978, kabla ya kuajiriwa jeshini.

No comments:

Powered by Blogger.