LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAFANYABIASHARA KAHAMA WAOMBA KUJENGEWA KIWANDA CHA SARUJI KANDA YA ZIWA.

Call 0784 699 668 Or 0754 806 640

Na Shaban Njia
Wafanyabiashara wa Saruji katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kujenga Kiwanda cha Saruji mkoani humo ili kupunguza ngarama za usafirishaji zinazowakabiri hivi sasa.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Ahmed Gulamrasul, kutoka Kampuni ya Agas Building Tanzania Limited amesema gharama wanazotumia kusafirisha saruji ni kubwa hivyo ni vyema kiwanda cha saruji kikajengwa kanda ya ziwa ili kupunguza gharama hizo.

“Mimi nilinunua tani 18,000 kutoka katika kiwanda cha Dangote Industry Limited kilichopo Mkoa wa Mtwara  tarehe 29/2/2016 sawa na mifuko 5,555 yenye thamani ya shilingi milioni 57.7 lakini mzigo niliupata  tarehe 05/03/016 jijini Dar es Salaam kwa kuletwa na usafiri wa Kampuni hiyo ya Saruji”, Alisema Gulamrasul kuelezea namna kulivyo na ugumu katika kusafirisha saruji haki kufika Kahama.

Alisema kuwa baada ya mzigo huo kusafirishwa kwenda kwenye magari kwa ajili ya kufikishwa Kahama, kulibainika  kuwa kuna jumla ya mifuko 685 ya  Saruji ambayo ilikuwa imeganda  yenye thamani ya shilingi milioni 35 hali ambayo baada ya kuwasiliana na viongozi wa juu wa Kampuni hiyo walisema airudishe.

Hata hivyo Mfanyabiashara huyo aliamua kuirudisha mifuko hiyo ili aweze kubadilishia mingine  baada ya hiyo kubainika kuwa imeganda na kuongeza kuwa tangu airudishe mifuko hiyo mpaka leo Kampuni hiyo haijaweza kumreshea mifuko mingine alioahidiwa kufidiwa.

Hata hivyo Gulamrasul alisema kuwa baada ya kufanya Mawasiliano na uongozi wa juu wa Kampuni hiyo wamekuwa wakimzungusha kumrejeshea mifuko hali ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa katika kumtia hasara na kuongeza kuwa hata wakifanya mawasiliano kwa njia simu wamekuwa hawapokei simu zake hali ambayo anaiomba Serikali kuingilia kati suala hilo.

Kwa upande wake Afisa utawala na Masoko wa Kampuni ya Dangote Industries Limited Gloria Mabada akijibu tuhuma hizo kwa njia ya Baruapepe alisema kuwa Kampuni hiyo tayari limekwisha ilipa Kampuni ya Agas Building Solution Limeted  ya Mjini Kahama kiasi cha shilingi milioni 4.3 kupitia akaunti ya mfanyabiashara huyo iliyopo katika kiwanda chake huku kiasi cha shilingi million mbili kikiwa kimebakia.

Nae Mfanyabiashara wa Saruji mjini Kahama Bhaiji Musa alisema kuwa suala la Kampuni ya Dangote kusafirisha bidhaa hiyo ikiwa imeganda lilikuwepo tangu siku za nyuma ikiwa ni pamoja na kuchelewelesha kufikisha mizigo kwa wateja.

No comments:

Powered by Blogger.