DK. JOHN POMBE MAGUFULI ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA WA CCM, AMCHAGUA TENA KINANA KUWA KATIBU MKUU.
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete wakiwapungia mikono wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM baada ya wajumbe hao Kumthibitisha kuwa Mwenyekiti wa awamu ya Tano Kwa kumpigia kura zote za ndiyo wajumbe waliopiga kura ni 2,398 ambapo hakuna kura zilizoharibika.
Mwenyekiti Dk. John Pombe Magufuli ameshinda kwa kwa kupigiwa kura zote 395, Lakini pia mwenyekiti huyo ameamua kuendelea na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Sekretarieti nzima iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA).

Viongozi wastaafu wakiwa katika mkutano huo kutoka kushoto ni Mzee John Samwel Malecela, Mzee Amani Abeid Karum, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Mohamed Gharib Bilal na Mzee Pius Msekwa.
Viongozi hao wakiwa katika meza kuu wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha TLP Ndugu Agustino Mrema akiwasliana na wake wa viongozi wastaafu.
Baadhi ya wajumbe wakishangilia mara baada ya mkutano huo kumthibitisha Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM.
Mgana Msindai akielekea jukwaani ili kutangaza nia yake ya kurejea CCM leo kwenye mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma.
Freddy Mpendazoe aliyekuwa mwanachama wa chama cha CHADEMA akitangaza nia yake ya kurejea CCM kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho uliofanyika mjini Dodoma leo.
No comments: