LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA MKOA WA MWANZA AWAONYA WAALIMU WADANGANYIFU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Vesterjtz wa BMG, Mwanza
Mkoa wa Mwanza, John Mongella (pichani), amewataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Mwanza, kupeleka idadi kamili ya wanafunzi wanaosoma katika shule za msingi na wale wa shule zote za sekondari mkoani humo, ifikapo agost tano mwaka huu.

Mongella ametoa agizo hilo jana, katika kikao cha pili cha Kamati ya ushauri Mkoa wa Mwanza (RCC), baada ya kupokea taarifa ya ya sekta ya elimu iliyokuwa na ombi la kuongezewa fedha kwa ajili ya kuendeshea shule, kufuatia shule nyingi kuelemewa na idadi kubwa ya wanafunzi.

Aidhaa Mongella alisema kumekuwepo na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya waalimu ili kuweza kupewa fedha nyingi za ruzuku ya kupitia mpango wa elimu bure ambazo hutolewa na Serikali.

"Kumekuwepo na uzidishaji wa idadi ya wanafunzi katika shule ili kuweza kupelekewa fedha nyingi kumbe ni udanganyifu wa walimu. Mwalimu anakuwa na idadi ya wanafunzi 500 lakini anaandika anawatoto 700 kinyume na maelekezo, sasa ifikapo agost tano  mwaka huu, wakurugenzi na wakuu wa wilaya muwe tayari mmeleta majibu mazuri ya idadi ya wanafunzi walioandikishwa na wanaosoma katika shule zenu. Alisema  Mongella.

Aidha alimuagiza Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa  TAKUKURU Mkoa mkoani Mwanza, Ernest Makale, kuhakikisha anafuatilia fedha zote zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ukarabati wa shule, huku akizitaka halmashauri zote kuhakikisha ifikapo Agost mbili mwaka huu, ziwe zimeishafanya kikao cha kutatua matatizo ya ardhi maana migogoro ya ardhi imekithiri mkoani Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.