LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA RIJK ZWAAN, CHUO CHA VETA NA UPENDO GROUP KWENYE MAONESHO YA NANENANE MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Kilimo cha Kisasa Kinalipa. Maonesho ya Wakulima na Wafugaji yanaendelea katika Kanda na Mikoa mbalimbali nchini tangu Agost Mosi mwaka huu. Mikoa ya Kanda ya Ziwa na hata mikoa jirani inakutana katika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Nyamhongolo Jijini Mwanza kwa ajili ya Maonesho hayo.

Kuna mambo mengi ya kujifunza katika maonesho hayo ikiwemo kujionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa hapa nchini pamoja na mashamba darasa katika sekta za Kilimo na Ufugaji na jinsi ya kuboresha bidhaa zitokanazo na mazao ya sekta hizo hadi kuingia sokoni.

Pichani ni Mwanahabari na Mjasiriamali Jijini Mwanza, Florah Magabe, kutoka Vijana Mwanza Succos na Tanzania Youth Enterpreneurship Organization TAYEO akiwa katika shamba darasa la Kampuni ya kutengeneza mbegu za kilimo ya RIJK ZWAAN.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, anatarajiwa kufungua maonesho hayo rasmi hii leo Agost 04,2016. 
Na BMG
Kutoka kushoto ni George Upina ambae ni Meneja wa Kampuni ya RIJK ZWAAN, Kanda ya Ziwa, akiwa na Beatus Kisus ambae Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vijana Mwanza Succos na Tanzania Youth Enterpreneurship Organization TAYEO (katikati) pamoja na Florah Magabe (kulia).
Kulia ni baadhi ya wananchi wakisaini kitabu cha wageni katika banda la Kampuni ya utengenaji wa mbegu za kilimo ya RIJK ZWAAN katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa. Kushoto ni Anania Josia kutoka kampuni hiyo akiwapa maelezo kuhusiana na kampuni hiyo na mbegu inazotengeneza.
Elimu juu ya mbegu za mazao ya mbogamboga ikitolewa kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza kwa mikoa Kanda ya Ziwa.
Anania Josia kutoka kampuni ya RIJK ZWAAN akionesha miongoni mwa mbegu bora za mazao ya mbogamboga (kabeji) yanayotengenezwa na kampuni hiyo
Hiki ni Kikundi cha Wajasiriamali kutoka Misungwi mkoani Mwanza. Kikundi hiki kinajulikana kwa jina la "Upendo Group", ni maarufu kwa utengenezaji wa Wine ya Rozera, Peanut Butter, Ungalishe wa soya, ulezi, mahindi na mchele, Asali mbichi, klipsi za viazi lishe na mengine mengi. Tembelea banda la kikundi hiki kwa elimu nzuri zaidi.
Banda ya Upendo group
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi VETA mkoani Mwanza, pia imeshiriki Maonesho ya Nanenane. Lengo ni kutoa elimu juu ya elimu na shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo.

"Tatizo ni upatikanaji wa vyuma vya alminiamu na stainless (vyuma visivyopata kutu) ni changamoto kwa hapa Tanzania katika utengenezaji wa mashine mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa mashine za kukamua juisi ya miwa". Anasema Yohana Wanga (wa pili kulia) ambae ni mmoja wa waalimu wa Veta mkoani Mwanza katika kitengo cha uchomeleaji.
Hii ni mashine ya kutengeneza juisi ya miwa. Kwa sasa soko la juisi ya miwa liko vizuri hivyo mashine hii ni nzuri kwa wajasiriamali
Majiko ya kuchomea nyama ni miongoni mwa elimu na shughuli zinazofanywa na Veta.
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.