LIVE STREAM ADS

Header Ads

MADIWANI NA WATENDAJI WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA TENDA ZA BARABARA MKOANI SIMIYU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Image result for SIMIYUNa Happy Severine, Simiyu.
Madiwani na watendaji wa Halmashauri wametakiwa kuacha kuingiza maslahi binafsi katika ujenzi wa miradi ya barabara ili kufanya miradi hiyo kusimamiwa na kujengwa katika kiwango kinachostahili.

Hayo yameelezwa na mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika katika ukumbi wa kanisa katolini mjini Bariadi.

Mtaka alisema kuwa ili miradi ya ujenzi wa barabara isimamiwe na kujengwa kwa viwango vinavyotakiwa ,madiwani na watendaji wasiwe sehemu ya wazabuni (wakandarasi)wa miradi hiyo ,kwani endapo hawatashiriki itakuwa rahisi kuwachukulia hatua wazabuni pale watakapokuwa wametekeleza chini ya kiwango.

“ninachoweza kuwaasa madiwani na watendaji wa halmashauri ni kuacha mara moja kujihusisha na tenda za zozote za halmashauri hususani za ujenzi wa barabara…kwani endapo watajihusisha itakuwa vigumu kwa wao kuwawajibisha pindi watakapobainika vibaya…Alisema

Aidha Mtaka  pia amewaasa wenyeviti wa halmashauri , kusimamia kwa umakini vikao vya baraza la madiwani ambavyo ni vya maamuzi juu ya matengenezo ya barabara ili vipaumbele vya kwanza viwe  ni sehemu korofi na madaraja.

Sambamba na hilo Mkuu huyo amewaomba viongozi  wa ngazi zote kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa alama za barabarani zilizowekwa na wakala wa barabara (Tanroad) pamoja na kuacha kupitisha mifugo kwenye barabara za lami ambayo inasababisha mmomonyoko wa udongo na kuzifanya barabara hizo zisidumu kwa muda mrefu.

Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini amesisitiza wahandisi wa Halmashauri kuhakikisha wanaweka alama katika mipaka ya hifadhi ya barabara ili iwe rahisi kutambua sehemu husika na kuepuka uvamizi wa maeneo.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la maswa Mashariki,Mhe.Stanslaus Nyongo kuna haja ya wakala wa barabara (Tanroad) kuwashirikisha kwa karibu wabunge wa mkoa wa Simiyu juu ya changamoto za utekelezaji wa mradi wa barabara kwa kiwango cha lami ambazo zinaunganisha mkoa na mikoa mingine .

Mhe Nyongo amesema endapo kutakuwa na taarifa za karibu mara kwa mara zitawawezesha kufanya  jitihada za kuzungumza na Waziri mwenye dhamana ili kipande cha Maswa hadi Bariadi chenye urefu wa kilomita 50 kitengewe fedha  kwani   barabara ya Mwigumbi-Maswa,Maswa-Bariadi ,Bariadi –Lamadi itakapokamilika itakuwa kiunganishi kizuri cha Mkoa na Mikoa mingine katika kuongeza uchimi .

Mkoa wa Simiyu una mtandao wa barabara zenye ukubwa wa kilometa 4,730.95 ambazo zimegawanyika katika makundi ya barabara kuu kilometa 334.74,barabara za Mkoa kilometa 532.30 ,barabara za wilaya kilometa 2420.5, za vijiji 141.76  kati ya hizo kilometa 2452zinakiwango cha lami, kilometa 2134.7 za kiwango cha udongo.

No comments:

Powered by Blogger.