LIVE STREAM ADS

Header Ads

MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAZINDUA VIFAA VYA USAFI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for image environmental pollutionNa James Salvatory - BMG Dar
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es salaam kwa kushirikiana na kampuni ya usafi ya Greenwastepro imezindua vifaa vipya vya kubebea takataka aina ya toroli za miguu mitatu yenye thamani ya shilingi milioni nane, lengo likiwa ni kurahisisha kazi ya usafi katika maeneo ya manispaa hiyo.

Akizungumza jana kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Nitupalele, afisa usafishaji na mazingira wa halmashauri hiyo, Abdons Mapunda, wakati akizindua mpango huo jijini humo alisema kuwa toroli hizo za kusukuma zitasaidia kuongeza ufanisi katika kazi bila kutumia nguvu nyingi ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kutengeneza matoroli 50.

Afisa huyo aliyataka makampuni mengine yanayojihusisha na masuala ya usafi kujenga tabia ya kuboresha mazingira katika manispaa zilizopo kwa kuwapatia vifaa vyenye ubora zaidi.


Kwa upande wake meneja mwendeshaji kutoka kampuni ya Greenwastepro, Abdalah Mbena, alisema toroli hizo zitaweza kusambazwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kariakoo,kisutu pamoja na kivukoni huku matarajio yakiwa ni kuongeza matoroli mengi zaidi ili kuondoa adha ya ubebaji takataka katika maeneo ya halmashauri hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.