LIVE STREAM ADS

Header Ads

MASHINDANO YA WUSHU KUNG-FU KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM MWEZI HUU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for WUSHU KUNG-FUNa James Salvatory BMG DAR
Rais wa mchezo wa Wushu Kung Fu nchini, Mwalam Mitete, amewaomba wananchi kujitokeza kwenye mashindano ya Wushu Kung Fu ambayo yatafanyika Jijini Dar es salaam Septemba 17 na 18 mwaka huu kwenye ukumbi wa uwanja wa taifa (Indoor Stadium).

Akizungumza jana na wanahabari Jijini Dar es salaam, Mitete alisema kupitia chama cha mchezo huo nchini, Tanzania Wushu Association pamoja na Ubalozi wa China nchini Tanzania, wameandaa mashindano ya tatu ya kitaifa ya mchezo wa Wushu Kung Fu ambapo hakutakuwa na kiingilio.

Aliongeza kwamba tofauti na mchezo huo, pia vyama mbalimbali vya sanaa za mapigano vimealikwa ili kujumuika pamoja kwenye mashindano hayo ambayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na balozi wa China nchini, wamealikwa.

Aidha alitanabaisha kwamba mashindano yatafungwa na Waziri wa Habari, Uamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye, akiambatana balozi wa China nchini na kukabidhi zawadi kwa washindi.

No comments:

Powered by Blogger.