CHANJO YAWASILI NCHINI, WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Andrew Chale
Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto tayari imepata chanjo ambazo zilikua pungufu hapa nchini kwa muda mrefu ambapo kwa sasa Wananchi watapatiwa huduma hiyo kuanzia sasa huku wakiombwa Wazazi na Walezi kupeleka watoto wao.
Kwa mujibu taarifa zilizotolewa na Serikali kuputia Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya Bwana Nsachris Mwamwaja amesema kuwa chanjo hizo zilizokuwa na upungufu mkubwa hazitasumbua upatikanaji wake kwa sasa baada ya kuwasili nchini.
“Tutegemee upungufu huu wa chanjo katika baadhi ya sehemu za nchi kuisha, Wizara inawaomba Wazazi na walezi kuwapeleka watoto ambao hawakupata chanjo wakakamilishe kupata chanjo zao.” Imeeleza taarifa hiyo kutoka kwa Mkuu huyo wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya.
Mkuu huyo amezitaja chanjo zilizokua na upungufu mkubwa kama zile za upungufu za Pepopunda (T.T) na Kifua Kikuu (BCG) na akaongeza kuwa zimewasili nchini kuanzia siku ya jana yaani Oktoba 03, 2016 na ameongeza kuwa siku ya kesho yaani Oktoba 5, 2016 Wizara itapokea chanjo za Polio (OPV) chanjo ambazo zinatarajiwa kusambazwa wiki hii nchini kote.
Aidha Bw Mwamwaja amewahimiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kushiriki vyema katika utoajiwa chanjo hizo.
“Waganga wakuu wa mikoa na wilaya kwa kushirikiana na waratibu wa chanjo wahakikishe chanjo zinasambazwa katika vituo vyote” ameongeza Bw Nsachris Mwamwaja katika taarifa hiyo.

No comments: