LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI BAADHI YA MAPINGAMIZI KWENYE KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA BUNDA MJINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Rose Jacob, Musoma
Jaji wa Mahakama kuu Tanzania, Noel Chocha, leo ametupilia mbali pingamizi liliowekwa na wakili wa wajibu maombi, Cosntantine Mtalemwa, dhidi ya shaidi namba moja Ester Bulaya katika kesi namba moja ya mwaka 2015 ya uchaguzi wa wa jimbo la Bunda mjini mkoani Mara.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa majira ya saa 7:00 mchana ambapo Jaji Chocha alinza kutoa ufafanuzi dhidi ya mabishano ya hoja yalijitokeza hapo octoba 12 mwaka huu kwa kueleza kile kilichosemwa na mawakili wa pande zote mbili.

Baada ya kuelezea melezo ya pande zote mbili Jaji huyo alisema amelikataa pingamizi hilo kutoka na  kanuni ya 23 ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kama ilivyofanyiwa malekebisho mwaka 2015,ambayo haimkatazi mjibu maombi kuleta au kutambulisha mambo mapya katika kiapo chake cha ushahidi dhidi ya hati yake ya utetezi hakama mambo hayo hayakuainishwa katika hati yake ya utetezi.

“Kufuatia kupitia kesimbalimbali zilizokuwa zimeisha kutolewa maamuzi  yanayoendana kesi hii maamuzi ya Mahakama yamelikatta pingamizi  lilowekwa na walili Cosntantine Mtalemwa aneyewawakilisah upande wa walalamikaji  la kutaka vifungu  namba 2,3,4,5,6,7 na 8 kuondolewa katika kiapo cha shahidi namba moja Estar Bulaya ambaye ni mlalamikiwa, hayataondolewa na kiapo chake kitapokelewa bila kupunzwa kitu chochote kwa mjibu wa kanuni ya 23 ya mwaka 2010,”alisema Jaji Chocha.

Vile vile  kiapo chote cha shahidi Ester Bulaya kitaingia katika kumbukumbu za Mahakama hivyo mtoa ushahidi ataulizwa maswali na mawakili wa walalamikaji kwa upana zaidi kutokana na upana wa mabo yaliyopo kwenye  kiapo chenyewe ikiwemo mambo mapya aliyoongezeka kwenye kiapo hicho.

Aidha baada ya Jaji kumaliza kutoa maamuzi hayo, alizieleza  pande zote mbili kuwa yoyote ambaye ajalidhika na maamuzi hayo anaweza kukata rufaa,akiihairisha kesi hiyo majira ya saa 8:45 mchana ikiwa na kutoa maaelekezo kwa shahidi huyo ataanza kutoa ushahidi Octoba 17 mwaka huu siji ya jumatatu.

No comments:

Powered by Blogger.