LIVE STREAM ADS

Header Ads

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF UMEENDELEA KUWAFIKIA WATU WENGI KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 Afisa Mwendeshaji  kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary akiwaeleza wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF ikiwa ni pamoja na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) ambapo mtu yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 anaweza kujiunga na kunufaika na mafao mengi.
 Baadhi ya viongozi na watumishi wa Hoteli ya Heritage wakiwa wanasikiliza kwa makini somo kutoka kwa  Afisa Mwendeshaji  kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary kuhusu mafao yatolewayo na Mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)
 Mmoja wa wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage akiwa anasoma jarida kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF
  Afisa Mwendeshaji  kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary akigawa vipeperushi na majarida yanayohusu mambo mbalimbali  juu ya mfuko huo
 Wafanyakazi wa Hotel ya Heritage wakiwa wanachukua fomu kwa ajili ya kujiunga na Bima ya afya ya NHIF itolewayo kwa Bei nafuu kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)
 Baadhi ya watumishi wa Hoteli ya Heritage Jijini Dar es salaam wakiendelea kusoma vigezo masharti na mambo mbalimbali juu ya Bima ya afya ya NHIF inayotolewa kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)
Wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage wakiendelea kupata maelezo juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka kwa  Afisa Mwendeshaji  kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary.
Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa 


Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wake wa uchangiaji wa Hiari (PSS) umeendelea kuyafikia makundi mbalimbali kujiunga na mpango huo.

Hayo yamesemwa na  Afisa Mwendeshaji  kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary alipokuwa akitoa maelezo na mafunzo juu ya mfuko huo na wafanyakazi wa  Hoteli ya  Heritage iliyopo Jijini Dar es salaam  ambapo pamoja  na kutoa maelezo juu ya mfuko huo na kutoa  elimu ya juu ya mpango huo wa uchangiaji wa  hiari ambapo  mwanachama atatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 ,  atakuwa huru kuchagua muda wa kuchangia kutegemea kipato chake huku kiwango cha chini kikianzia Shilingi 10,000 ambayo mwanachama anaweza kulipia kupitia benki na huduma za simu.

Bwana Hadji alisema kuwa mpango huo wa hiari unakaribisha raia na mtu asiye raia bila kusahau mjasiriamali na mfanyakazi wa serikali  na kuongeza kuwa  mwanachama anayejiunga katika mfuko huo huweza kupata mafao ya aina sita ambayo ni; Fao la Elimu, Fao la Ujasiriamali, Fao la Uzeeni, Fao la Kifo, Fao la Ugonjwa/Ulemavu, Fao la Kujitoa, na Fao la Matibabu.

Akifafanua kuhusu Fao la Matibabu, Bwana Hadji alisema kuwa kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari wanashirikiana na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo mwanachama ataweza kupatiwa huduma bure katika hospitali na maduka ya madawa yaliyosajiliwa na NHIF kote nchini.

“Mwanachama anaweza kuwasajili pia wategemezi wake watano na kuendelea kupata mafao yetu bila shida yoyote,” alisema Hadji.

Wakizungumza kwa nyakati mbalimbali wafanyakazi hao walionesha kufurahia unafuu wa mfuko huo na kuwataka PSPF kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wananchi wengi wajiunge kwa kuwa hupoteza fedha nyingi ambazo wangeweza kuziokoa kwa kujiunga na mfuko huo.

Aidha Hadji aliwaambia wafanyakazi  hao kuwa PSPF ina wawezesha  wanachama wake na jamii kwa ujumla kumiliki nyumba zilizopo Dar , Morogoro, Tabora, Mtwara, Shinyanga na Iringa ambapo wataweza kununua kwa mkopo au malipo ya mara moja pamoja na mikopo ya viwanja vilivyo sehemu mbalimbali nchini.

No comments:

Powered by Blogger.